Kpah Sherman
MSHAMBULIAJI mpya wa Yanga, Kpah Sherman sasa ni ruksa kucheza katika
Ligi Kuu baada ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kuthibitisha
kwamba hati yake ya uhamisho kumruhusu kucheza soka nchini tayari
imeshafika.
Aidha, wakati Sherman akiwa na uhakika wa kuitumikia klabu hiyo, TFF
imethibitisha kuchelewa kwa hati ya uhamisho ya kiungo mpya wa Yanga,
Emerson de Oliviera Roque ambaye aliombewa ITC ili kuitumikia timu hiyo.
Licha ya kuwepo kwa taarifa za kukatwa kwa mchezaji huyo na nafasi
yake kupewa aliyekuwa mchezaji wa Simba, Amisi Tambwe, Mkurugenzi wa
Mashindano wa TFF, Boniface Wambura alisema jana kuwa ITC hiyo
haijafika.
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz,
ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali
na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715
221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.
“ITC ya Emerson haijafika, lakini tayari maombi yalikwenda na
kilichokuwa kinasubiriwa na majibu ya Shirikisho la Soka Brazil,”
alisema Wambura.
Mchezaji mwingine ambaye hajapata ITC ni Juuko Musheed aliyesajiliwa
Simba hivi karibuni ambaye pia maombi yake yanasubiriwa kutoka Victoria
University ya Uganda.
Kwa mujibu wa Wambura, maombi ya ITC zao yalitakiwa kufika jana
mchana na kwamba iwapo yatafanikiwa Yanga italazimika kukata mchezaji
mmoja, ili wabaki watano wanaotakiwa kwa mujibu wa kanuni.
Aliwataja wachezaji wengine waliopata ITC kuwa ni Abdul halim Humud
aliyetoka Sofapaka kwenda Coastal Union, Brian Majwega aliyetoka KCC ya
Uganda kwenda Azam FC, Dan Sserunkuma kutoka Gor Mahia kuja Simba, Simon
Sserunkuma kutoka Victoria University aliyesajiliwa Simba na Paschal
Wawa kutoka El Merreikh kwenda Azam FC.
Kuhusu wachezaji ambao wamekwenda kwa mkopo na waliosajiliwa, Wambura
alisema itajulikana baadaye kwa vile maombi ya wachezaji hao hupitia
mtandao na sio makaratasi tena.
Wambura alisema kwa mujibu wa Kanuni, wachezaji wasiozidi watano ndio
ambao huruhusiwa kwenda kwa mkopo kutoka timu moja kwenda nyingine na
hiyo ni kwa timu zote kuanzia Ligi Daraja la Kwanza. Alisema wiki ijayo
Kamati ya Sheria ya TFF itakaa kuangalia timu zilizozingatia kanuni za
uhamisho na ambazo hazijazingatia.
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz,
ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali
na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715
221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.
No comments:
Post a Comment