Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.
Kabla ya kuwa Mwanasheria Mkuu, alikuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya
Tanzania tangu 2007 mpaka 2009. Mwaka 2004 hadi 2006 alikuwa ofisi ya
Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Werema alihitimu Shahada ya kwanza ya Sheria katika Chuo Kikuu cha
Dar es Salaam mwaka 1984 na shahada ya pili ya sheria mwaka 1993 katika
Chuo Kikuu cha American, Washington DC nchini Marekani.
Kisa ni Escrow “Katika barua yake kwa Mheshimiwa Rais Kikwete, Jaji
Werema amesema kuwa ameomba kujiuzulu kwa sababu ushauri wake kuhusu
suala la Akaunti ya Tegeta Escrow hakueleweka na umechafua hali ya
hewa,” imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.
Taarifa iliongeza kuwa Rais Kikwete amemshukuru Jaji Werema kwa
utumishi wake ulioongozwa na uaminifu na uadilifu. Katika Mkutano wa 16
na 17 wa Bunge uliohitimishwa Novemba 28, mwaka huu, moja ya mambo
makubwa yaliyoibuka na kuzua mjadala mzito ni sakata la uchotwaji wa
fedha katika akaunti ya Escrow, kiasi cha kutaka Mwanasheria Mkuu wa
Serikali, baadhi ya mawaziri na watendaji Serikali wajiuzulu.
Bunge liliazimia Jaji Werema kushughulikiwa kwa mujibu wa sheria
kutokana na kuipotosha Serikali kuhusu malipo ya Sh bilioni 306 kutoka
akaunti ya Tegeta Escrow, akishauri fedha hizo zilipwe kwa Kampuni ya
IPTL iliyo na mkataba wa ufuaji umeme na Tanesco bila ya kukata kodi.
Hata hivyo, Jaji Werema hakusalimu amri wakati Bunge likijadili
tuhuma dhidi yake, akisema anaamini alichofanya na kutaka abebeshwe
msalaba na wakati fulani alishiriki kupendekeza jinsi ya kufikia
maazimio ya Bunge dhidi ya watuhumiwa.
Aidha, alilalamikia uamuzi wa Bunge uliokuwa umependekeza yeye na
baadhi ya vigogo wachukuliwe hatua, akidai kuwa haukuwa wa haki kwa wote
waliotuhumiwa na ulifanywa kwa hasira na kufuata mkumbo.
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz,
ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali
na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715
221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.
Akizungumzia maazimio ya Bunge katika sakata la uchotaji wa fedha
hizo, Jaji Werema alisema: “Kilichofanywa na Bunge ni mob justice
(uamuzi wa kufuata mkumbo) kwa sababu hata waliowatuhumu, hawakupewa
nafasi ya kujieleza.
(Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Anna) Tibaijuka na
(mmiliki wa hisa za IPTL, James) Rugemalira hawakusikilizwa lakini
wamehukumiwa… ilionekana dhahiri jinsi Bunge linavyoingilia uhuru wa
Mahakama kwa kutoizingatia hukumu ya Jaji (John) Utamwa.
“There was no justice at all (hakukuwa na haki kabisa). Bado
haijathibitika ukweli kuhusu fedha zile kama ni za umma au la. Ninyi
waandishi bado mna nafasi ya kufanya uchunguzi ili muwaeleze wananchi
ukweli kuhusu wasichokijua,” Akijizungumzia yeye mwenyewe, alisema:
“Nitasimama mwenyewe kujitetea, lakini nawaomba, tafadhalini
msichafuane.Acheni kutoa makaratasi na vitabu. Kesi hii inaendeshwa
kiuchunguzi. Tuache kuchafuana.”
Aidha, katika hilo, alisisitiza kuifuata Katiba ya nchi akisema ndio
mwongozo unaokubalika. Werema alitaka pia Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi
Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) iueleze umma ili kuondoa sintofahamu
iliyopo juu ya mmiliki halali wa fedha zilizokuwamo katika akaunti hiyo.
Bunge lilihitimisha mjadala wa kashfa ya akaunti ya Tegeta Escrow,
kwa kupitisha maazimio manane, ikiwa ni pamoja na kuwawajibisha
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Waziri wa Nishati na Madini, Profesa
Sospeter Muhongo na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,
Profesa Anna Tibaijuka.
Bunge hilo pia lilipendekeza kuwajibishwa kwa wajumbe wa Bodi ya
Wakurugenzi wa Shirika la Umeme (Tanesco) na lilipendekeza kuwavua
nyadhifa zao wenyeviti watatu wa kamati za kudumu za Bunge ambao ni
mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini, Victor Mwambalaswa, Kamati ya
Katiba, Sheria na Utawala, William Ngeleja na Kamati ya Bajeti, Andrew
Chenge.
Akisoma maazimio hayo, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Hesabu za Serikali (PAC), Zitto Kabwe alisema kuwa baadhi ya watu
waliochukua fedha hizo ni viongozi wa umma na maofisa wa Serikali kama
mawaziri, majaji, wabunge, wenyeviti wa kamati za Bunge, wakuu wa
taasisi za umma, viongozi wa dini, mawakili wa kujitegemea na watu
binafsi.
Maazimio yaliyopendekezwa ni pamoja na kulitaka Jeshi la Polisi na
vyombo vingine vya ulinzi na usalama kuchukua hatua stahiki kwa mujibu
wa sheria za nchi ili kukabiliana na kile kinachoonekana kuwa ni rushwa
katika utoaji wa mabilioni yaliyokuwemo katika akaunti hiyo.
Azimio la tatu lilikuwa ni kuzitaka Kamati za kudumu za kuwavua
nyazifa zao za wenyeviti wa kamati husika za Bunge kabla ya mkutano wa
18 wa Bunge hilo na la nne likiwa ni kumwomba Rais aunde tume ya kijaji
kuchunguza tuhuma za ukiukwaji wa maadili dhidi ya Jaji Aloysius
Mujulizi na Jaji Profesa Eudes Ruhangisa wa Mahakama Kuu ya Tanzania.
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.
No comments:
Post a Comment