Taarifa zilipatika sasa hivi ni kuwa Paroko wa
Kanisa la Katoliki Minara Mirefu Zanzibar, Evarist Mushi amefariki dunia
baada ya kupigwa risasi saa 1.00 asubuhi na kufariki kabla hajafika
hospitali ya Minazi Mirefu. Paroko huyu amepigwa risasi akishuka katika
gari lake wakati akienda kuendesha ibada ya saa 3.00 leo.
Kwa siku za hivi karibuni
kumekuwako na vitisho vya wazi wazi dhidi ya wakristu huko visiwani
Zanzibar ambapo inaelezwa kuwa jeshi la polisi halijafanya juhudi yoyote
kuzuia tishio hili. Kumekuwapo na vipeperushi vinavyodai kuwa kupigwa
risasi kwa padre Ambrose sio mwisho wa mapambano.
Taarifa hizi zimeripotiwa direct toka Zanzibar.
Taarifa hizi zimeripotiwa direct toka Zanzibar.
R .I.P
SOURCE WAPO RADIO
SOURCE WAPO RADIO
No comments:
Post a Comment