Mwanariadha wa Afrika Kusini ambaye ana
ulemavu wa miguu na ambaye ni mashuhuri sana katika riadha ulimwenguni
Oscar Pistorius, anatarajiwa kufika mahakamani leo kwa mara ya pili, ili
kuwasilisha ombi la kuwachiwa kwa dhamana, baada ya kushtakiwa kwa
kumuuwa mchumba wake.
Waendesha mashitaka
wanatarajiwa kupinga ombi lolote la dhamana katika kikao cha leo.
Kukamatwa kwa mwanariadha huyo wa Olimpiki
ya walemavu mwenye umri wa miaka 29 kumewashangaza mamilioni ya watu
ulimwenguni ambao walimwona kama shujaa aliyeweka kando ulemavu wake na
kushindana na watu wasio na ulemavu katika Olimpiki.
Mpenzi wake, mwanamitindo Reeva Steenkamp
alipatikana akiwa amepigwa risasi na kuuawa nyumbani kwa mwanariadha
huyo mjini Pretoria mapema Alhamis iliyopita, huku ripoti za mwanzo
zikisema Pistorius huenda alimdhania kuwa mwizi.
Hata hivyo polisi inasisitiza kuwa
Steenkamp ambaye atazikwa leo, aliuawa na zaidi ya risasi moja, na
Pistorius ndiye mshukiwa pekee na kwamba majirani walisikia vurugu hapo
kabla.
No comments:
Post a Comment