MJUMBE wa Halmashauri
Kuu ya
Taifa (NEC) ya CCM, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete ametoboa
siri kwamba
mumewe, Rais Jakaya Kikwete pamoja sura yake kujawa haiba ya ucheshi wa
mara kwa mara lakini kwa tabia ana hasira.
Amesema, Rais Kikwete
hukasirika sana anapoona au
kusikia mtu au mtendaji katika Chama au serikali anafanya mambo ya hovyo
au ya kizembe hasa katika masuala ya kazi.
Mama
Salma Kikwete ametoboa siri hiyo, leo Februari 18, 2013, kwenye mkutano
wa hadhara uliofanyika kwenye kijiji cha Kikwetu Kata ya Mbanja akiwa
katika ziara ya kukagua, kuimarisha uhai wa chama, kukagua utekelezaji
wa ilani ya Chama na kuwashukuru wana-CCM wa Lindi mjini kwa kumchagua
kuwa mjumbe wao wa NEC.
"Siyo kweli kwamba
Rais Jakaya Kikwete si mkali,
japokuwa ana sura yenye haiba ya ucheshi wa mara kwa mara kwa kila mtu,
lakini ana hasira, tena sana pale mtendaji au mtu yeyote anapombaini
kwamba anafanya mambo ya hovyo hovyo au
ya kizembe katika kazi za Chama au
serikali yake", alisema Mama Salma Kikwete.
Mama Kikwete akitoa
ufafanuzi, baada ya
mshereheshaji mmoja kwenye mkutano huo, Mwenyekiti wa CCM wa wilaya ya
Lindi mjini Muhsin Ismail, kusema kwamba Rais Jakaya Kikwete ni mpole wa
kupindukia na kuuliza umati wa wananchi waliokuwa kwenye mkutano huo
kwamba je ni nani amewahi kumuona amenuna.
"Natoa ofa kama hapa
kuna mtu aliyewahi kumuona
mpendwa wetu, Rais Kikwete amenuna anyooshe mkono. Akitokea ntampa sh.
elfu moja hapa hapa... Kwa mara ya kwanza, ya pili unaona hakuna",
alisema Muhsini.
No comments:
Post a Comment