Balozi
Joel M Nheleko wa Swaziland nchini Ubeligiji, ambaye alikuwa Rais wa
Mabalozi wa Afrika nchini Ubeligiji aliyemaliza muda wake, akimkabidhi
Balozi wa Tanzania Dk. Diodorus Kamala mfuko wenye vitendea kazi kama
ishara ya kumkabidhi Urais wa Mabalozi wa Afrika Ubeligiji jijini
Brussels.
Balozi
wa Tanzania nchini Ubeligiji, Dk. Diodorus Kamala ameteuliwa na
mabalozi wa nchi za Africa wanaoziwakilisha nchi zao nchini humo kuwa
Mwenyekiti wao.
Balozi
Kamala amepokea uenyekiti huo kutoka kwa Balozi wa Swaziland nchini
Ubeligiji, Joel Nheleko aliyemaliza muda wake. Tanzania itashikilia kiti
hicho kwa muda wa miezi sita hadi Julai 1, 2013.
“Nimefurahi
kupewa heshima hii, na naamini nitaitumia fursa hii kufahamiana vizuri
na mabalozi wenzangu na kuvutia fursa za kiuchumi kwa nchi yetu,”
alisema Balozi Kamala.
Wakati
huo huo, juzi mabalozi wa nchi tano zinazozunguka Bonde la Ziwa
Tanganyika, walimchagua Balozi Kamala kuwa mwenyekiti wao.
Nchi
wanachama wa Bonde la Ziwa Tanganyika ni Burundi, Rwanda, Tanzania,
Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo na Zambia.
Nchi
hizi zimeunganisha nguvu kutafuta wafadhili kwa ajili ya maendeleo ya
Bonde la Ziwa Tanganyika, ambapo eneo la bonde hili lenye wakazi wastani
wa milioni 40 wanalenga kuliendeleza kwa ajili ya kujenga miundombinu,
kurahisisha usafiri na usafirishaji, kujenga reli mpya na kuendeleza
utalii.
Chini
ya mpango huu wanalenga pia kuboresha viwanja vya ndege vya nchi
wanachama vya Mbala, Kalemie, Bujumbura, Kigoma na Kasanga kwa nia ya
kurahisisha usafiri wa anga katika ukanda huu.
Dk.
Kamala amekabidhiwa jukumu la kuratibu mpango huu na kwa pamoja
watatafuta fedha kutoka kwa wafadhili kwa ajili ya mradi huu.
No comments:
Post a Comment