Mama
Mwili wa mke wa aliyekuwa rais wa
Kenya Mwai kibaki , mama Lucy Kibaki umewasili leo alfajiri mjini
Nairobi ukitokea London Uingereza na kutumbukiza taifa zima katika
kipindi cha maombolezi.
Mabaki ya bi Kibaki yalilakiwa katika
uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta na rais Uhuru Kenyatta Naibu wake
William Ruto na viongozi na wakenya wa haiba mbalimbali mwendo wa saa
kumi na moja. Ndege iliyoileta familia ya rais Kibaki ilitua saa kumi na moja na dakika tatu na kupewa hadhi ya kitaifa.
Kwaya aliyoipenda wakati wa maisha yake ya Mama Lucy ndio
iliyowaongoa waombolezaji wakati jeneza lake lililofunikwa na bendera ya
taifa ilipotolewa kwenye ndege hiyo ya Kenya Airways na wanajeshi wa
jeshi la Kenya.
Huzuni ilighubika umati wa viongozi waliofika uwanjani kuulaki mwili wake. Machozi yaliwalengalenga huku baadhi yao walioshindwa kustahimili waliangua kilio. Jeneza hilo liliwekwa kwenye hema ndogo kabla ya kasisi Dominic Wamugunda kuongoza misa fupi ya wafu.
Kisha mwili huo ukapelekwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti ya Lee Funeral. Msemaji
wa serikali bwana Eric Kiraithe amesema kuwa tarehe kamili ya mazishi
itatangazwa baadaye kutokana na itifaki baada ya serikali kuamua kumpa
mazishi ya kitaifa.
Hata hivyo vitabu vya risala za rambirambi vitafunguliwa katika
kanisa la Holy Family Basilica, na Consolata Shrine pamoja na afisi za
serikali kote nchini. Mama Lucy, 82 aliaga dunia jumanne iliyopita
katika hospitali ya Bupa Cromwell iliyoko London Uingereza alikokuwa
amepelekwa kwa matibabu ya ziada.
Lucy alipata umaarufu kwa kumchapa kofi mpiga picha mmoja mwaka 2005
wakati alipovamia afisi za kituo kimoja cha habari mwaka
akiwaamekasirishwa na jinsi habari moja ilivyoandikwa. Katika
kumbukumbu ya kumhenzi bi Kibaki rais wa Kenya Uhuru Kenyatta
alimsifu kwa jukumu lake kukabiliana na ugonjwa wa ukimwi nchini Kenya.
Kenyatta alimrithi mumewe Kibaki ambaye alitawala kati ya mwaka 2002-
2013.
Rais
Kenyatta alitangaza kuanza rasmi kwa siku tatu za maombolezi
alipochapisha picha hizi kwenye mtandao wake wa Facebook. Aidha
alitangaza bendera zote zipeperushwe nusu mlingoti katika muda huu wa
maombolezi.
1 comment:
After checking out a few of the blog articles on your web page, I really appreciate your way of blogging.
I saved it to my bookmark site list and will be checking back soon. Please visit my website as well and let me know your opinion.
Post a Comment