Wapiganaji wa Kiislamu wa Somalia, Al Shabab wanasema wamewauwa wanajeshi wa serikali zaidi ya 30. Al
Shabab, wanadai kutekeleza mauaji hayo walipoteka tena kijiji cha
Runorgood, Kaskazini-Mashariki mwa mji mkuu wa Somali Mogadishu.
Wenyeji wa kijiji hicho wamethibitisha, kwamba kijiji chao kinadhibitiwa tena na wanamgambo wa Al Shabab.
Wapiganaji hao walikuwa wametimuliwa kutoka kijiji hicho hapo jana. Kwengineko
nchini Somalia, watu kama watatu waliuwawa, kwenye shambulio la bomu,
katika soko la mifugo huko Qoryoolay, inavoelekea shambulizi hilo
lililengwa maafisa wa kukusanya kodi wa serikali.
No comments:
Post a Comment