Shirika
moja la kimataifa la kutetea haki za binadamu linasema kuwa zaidi ya
watu mia moja wamefariki kutokana na njaa pamoja na maradhi katika kambi
moja ya kijeshi katika Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.
Shirika
hilo Human Rights Watch, limesema kuwa watu hao ambao walikuwa
wapiganaji wa zamani na wake zao pamoja na watoto walihamishwa katika
kambi nyingine iliyotengwa Kaskazini mwa DRC.Ilikuwa baada ya wao kujisalimisha kutoka kwa kundi la wapiganaji Mashariki ya nchi.
Walipokea chakula kidogo na huduma ya afya baadhi wakiponea kifo kwa kuiba chakula kutoka kwa mashamba ya wakulima.
Serikali ya DRC inasema kuwa inachunguza ripoti hiyo. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
No comments:
Post a Comment