Saturday, November 22, 2014

CHAMA TAWALA ZAMBIA WAMTIMUA KAIMU RAIS CHAMANI

Scott alichukua usukani baada ya aliyekuwa Rais Michael Sata kufariki 
 
Chama tawala nchini Zambia (PF) kimemtimua kaimu rais wa nchi hiyo Guys Scott kutoka chamani na kuvunja utaratibu wa katiba.
Taarifa hii ni kwa mujibu wa msemaji wa chama hicho.
''Amekuwa akiwaajiri na kuwafuta watu kazi ovyo na pia bila ya kushauriana na kamati kuu ya chama,'' amesema Malozo Sichone.
Bwana Scott, ambaye licha ya hatua hiyo ataendelea kuwa mwanachama wa chama hicho, ataendelea kuhudumu kama kaimu rais hadi uchaguzi utakapofanyika tarehe 20 Januari.
Scott aliteuliwa kuwa kaimu rais kufuatia kifo cha hayati Rais Michael Sata aliyefariki mwezi jana. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...