Rashid Mvungi akimuangalia mtoto wake Nasrah Rashid (4) ambaye ni
mlemavu wa viungo aliyefungiwa chumbani na kufichwa kwenye boksi bila ya
kufanyiwa usafi tangu akiwa na umri wa miezi tisa.
Morogoro. Zimeibuka taarifa
kwamba mtoto aliyekuwa amefungiwa kwenye boksi kwa miaka minne na mama
yake mkubwa, Nasra Rashid (4) alikuwa na kaka aliyefahamika kwa jina la
Nasoro ambaye hadi sasa hajulikani mahali halipo.
Wakati polisi ikisema imefurahi kupata taarifa
hizo na kwamba itazifanyia kazi, habari zilizopatikana jana kuhusu hali
ya Nasra zimesema atafanyiwa vipimo 18 ili kubaini hali ya afya yake.
Vipimo vya awali, vimebaini kuwa amevunjika mifupa ya mikono na miguu na
kwamba atapelekwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa matibabu zaidi.
Kuhusu kaka yake, baadhi ya majirani wa nyumba
aliyokuwa anaishi mama mzazi wa Nasra enzi za uhai wake walidai kuwa
Mariamu alikabidhiwa watoto wawili kuwalea baada ya mama yao kufariki
dunia.
Mmoja wa majirani hao, Ramadhani Mansuri alisema
wakati mama mzazi wa Nasra akiishi eneo la Mjimpya alikuwa na watoto
wawili akiwamo Nasoro ambaye aliachwa akiwa na umri kati ya miaka 14-15.
Vipimo
Ofisa Ustawi wa Jamii, Mkoa wa Morogoro, Oswin
Ngungamtitu alisema taarifa alizopata kutoka kwa madaktari zinasema kuwa
mtoto huyo atafanyiwa vipimo 18 ili kubaini hali ya afya yake.
Akizungumzia matokeo ya vipimo vya awali, Mganga
Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro, Dk Rita Lyamuya alisema
haijafahamika sababu za kuvunjika kwa mifupa hiyo. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz
Dk Lyamuya alisema jana kwamba, mtoto huyo
ameshafanyiwa vipimo vingine kadhaa ambavyo vinaonyesha kwamba
anasumbuliwa na homa ya mapafu (pneumonia) na utapiamlo unatokana na
kukosa lishe bora.
“Tulilazimika kumfanyia vipimo hivyo vya awali kwa
sababu alikuwa anaonekana kama anayeugulia maumivu, kwa hiyo vipimo
vingine vitaendelea kufanywa kadri tutakavyoona inahitajika,” alisema Dk
Lyamuya.
Alisema kipimo cha X- Ray ndicho kilichoonyesha
kuvunjika kwa mifupa yake ya miguu na mikono na kwamba hali hiyo ndiyo
inayosababisha ashindwe kusimama na kutembea.
“Wakati anafikishwa hapa hospitalini alikuwa
amebanwa na kifua na alikuwa anashindwa kupumua vizuri. Ilitulazimu
kumwekea mashine ya oksijeni ili imsaidie kupumua, lakini sasa hali yake
inaendelea vizuri na tayari tumeondoa mashine, anaendelea na matibabu
mengine,” alisema.
Mbali na tiba, Nasra pia alifanyiwa usafi wa mwili
wake ambao ulikuwa mchafu kutokana na kutoogeshwa kwa muda mrefu na
sasa inaelezwa kuwa yuko kwenye hali ya kuridhisha na wasamaria wema
wameanza kujitokeza kumpa misaada ya nguo na chakula.
Na Mwananchi
Mjomba wa Nasra
Akizungumzia tukio hilo, Kaka wa Mariam, Mohamed
Said alisema baada ya dada yake kufariki dunia, Nasra alianza kulelewa
na mama yake mkubwa kutokana na baba yake mzazi kushindwa kutoa
ushirikiano.
“Mimi hali yangu ya maisha ni ngumu sana
nisingeweza kumlea Nasra kwa hiyo dada (Mariamu), aliamua kumchukua
amlee na naamini alikuwa akimhudumia kwa kumpa chakula na mahitaji
mengine, lakini cha kushangaza juzi napata taarifa kuwa amekamatwa kwa
kosa la kumfanyia vitendo vya kikatili mtoto Nasra,” alisema Said. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz
Said alisema mtoto huyo alizaliwa akiwa na uzito
mdogo na afya yake ilianza kudhoofika wakati mama yake alipokuwa mgonjwa
na baada ya kufariki dunia, viungo vya Nasra vilionekana kulegea na
kushindwa kutembea na kusimama.
“Kabla ya kifo cha mama yake, Nasra aliumwa sana,
lakini dada Mariamu alimlea vizuri na baada ya kugundua kuwa na ulemavu
alijitahidi kumfanyisha mazoezi ya kumsimamisha lakini mtoto mwenyewe
alikuwa anagoma, alipolazimishwa alikuwa analia sana, hivyo alikuwa
anakaa tu mahali pamoja na kujisaidia haja ndogo na kubwa hapohapo,”
alisema Said.
Alisema taarifa kwamba Nasra alikuwa akiishi
kwenye boksi na kuteswa, si za kweli kwani licha ya kumlea, Nasra dada
yao alishawahi kuwalea watoto wengine wa ndugu zao bila ya kuwafanyia
vitendo vya aina hiyo.
Alisema familia haitaweza tena kumlea mtoto huyo,
kwani imepatwa na hofu ya kupata lawama kama aliyoipata dada yake, hivyo
wanaiachia Serikali kumlea mtoto huyo au baba yake ambaye ni mtumishi
wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro.
Kuhusu malezi, Ngungamtitu alisema: “Tumeongea na
Rashid Mvungi ambaye ni baba mzazi wa Nasra na yeye amesema itakuwa
vigumu kumchukua kwenda kumlea kwa sababu alimzaa nje ya ndoa na
hakuwahi kumwambia mke wake mpaka tukio hilo lilivyotokea. Hatuwezi
kumlazimisha.”
Uchunguzi
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, Leonard
Paul alisema uchunguzi wa tukio hilo unaendelea na kwamba jeshi hilo
limefunga chumba cha mtuhumiwa kwa ajili ya usalama na kuepuka
kuharibika kwa ushahidi wa mazingira.
Alisema jeshi lake litashirikiana na Ofisi ya
Ustawi wa Jamii kuhakikisha kuwa Nasra anakuwa salama hospitalini na
kwingineko atakakopelekwa kwa sababu mbalimbali.
Nasra aligundulika akiwa amewekwa katika boksi nyumbani kwa mama yake
mkubwa, Mariamu Said, mkazi wa Kiwanja cha Ndege, Morogoro aliyekuwa
akimlea. Hivi sasa, Mariam pamoja na mumewe, Omar Mtonga wanashikiliwa
na polisi kwa kumficha mtoto wa huyo kwenye boksi kwa miaka minne. Mama
yake Nasra alifariki wakati mwanaye huyo akiwa na umri wa miezi tisa. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo TzNa Mwananchi
No comments:
Post a Comment