VIDEO Queen maarufu Bongo, Agnes Gerald
‘Masogange’ ambaye muda mwingi amekuwa akiishi Afrika Kusini ameelezea
jinsi maisha ya Bongo yalivyomchosha huku usumbufu anaopata kutokana na
makalio yake makubwa ikiwa moja ya sababu.
Akipiga
stori mwandishi wetu, Masogange alisema umbile lake hilo limekuwa
likimfanya akose amani anapokatiza mitaani, tofauti na Sauzi ambako
wanawake wengi wamefungashia huku yeye akionekana ‘cha mtoto’.
“Muda
mwingi niko Sauzi, Bongo miyeyusho na hili umbo langu nimekuwa
nikisumbuliwa sana na wanaume lakini Sauzi hili langu la kawaida, wengi
wamefungashia ile mbaya, kwa hiyo muda mwingi nitakuwa huko, huku
nitakuwa nakuja na kuondoka,” alisema Masogange.
No comments:
Post a Comment