KAMATI ya Ulinzi na
Usalama Mkoa wa Mbeya limepiga marufuku maandamano yoyote kufanyika
Mkoani hapa yenye lengo la kushinikiza Raisi Kikwete kumfukuza kazi
Waziri wa Elimu kutokana na matokeo mabaya ya kidato cha nne.
Maandamano hayo
yalipangwa kufanywa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo( CHADEMA)
Machi 25, Mwaka huu, ambayo yamepangwa kuhusisha Mikoa yote ya Nyanda
za Juu Kusini na kufanyika Jijini Mbeya kwa lengo hilo.
Akitoa taarifa ya
Kamati hiyo kwenye Mkutano wa ushauri wa Mkoa (RCC),Kaimu Mkuu wa Mkoa
wa Mbeya Dk. Norman Sigalla amesema kamati hiyo ilikaaa Machi 19, mwaka
huu na kuamua kuwa hakuna mantiki ya kufanyika kwa maandamano hayo.
Amesema sababu
iliyoonekana ni kwamba tayari tume imeshaundwa kuchunguza madai hayo
hivyo hamna sababu ya watu kuandamana kushinikiza waziri kujiuzulu ili
hali kamati itakuja na majibu juu ya kile kilichosababisha matokeo kuwa
mabaya.
Sigalla amesema kamati
ya Ulinzi na Usalama imeona kuwa kuendelea kufanya maandamano soyo
ufumbuzi wa matatizo bali yataathiri shughuli za kujitafutia kipato kwa
wananchi wa kawaida pamoja na usalama wa mali.
Ameongeza kuwa usalama
wa Wananchi wa Mkoa wa Mbeya utaathirika kutokana na wanaotarajiwa
kufanya maandamano hayo wamehamasishwa kutoka mikoa ya Iringa, Njombe,
Ruvuma ambako kutajaza idadi kubwa ya watu.
Amesema kamati pia
inaamini kuwa maandamano ya aina hiyo yanaweza kusababisha uvunjifu wa
amani hivyo kamati inapiga marufuku maandamano ya aina yoyote kufanyika
Mkoani Mbeya na kuongeza kuwa yapelekwe maeneo mengine.
Aidha ametoa rai kwa
vikundi vya kisiasa, kijamii na vikundi vya dini kuweka mbele maslahi ya
wananchi kwa kuhimiza kujitafutia vipato kutokana na fursa za maendeleo
zilizopo.
Hata hivyo Mwenyekiti
huyo wa kamati ya Ulinzi na Usalamaya Mkoa ameviagiza vyombo vyote vya
Ulinzi na usalama kuendelea kuhakikisha kwamba Mkoa wa Mbeya unaendelea
kuwa tulivu na amani ambayo itawezesha wananchi kuendelea na shughuli za
kujiongezea kipato bila bugudha yoyote.
Maandamano hayo
yamepangwa kufanyika Machi 25, Mwaka huu kufuatia Mkutano wa Hadhara
uliofanyika hivi karibuni wa Chadema katika Viwanja vya Shule ya Msingi
RuandaNzovwe Ilomba Jijini Mbeya Februari 28, Mwaka huu, ambapo
Mwenyekiti wa Chama hicho taifa Freeman Mbowe aliagiza kufanyika kwa
maandamano hayo kwa namna yoyote ile.
Pia katika kuhakikisha
dhana hiyo inatimia Mwenyekiti huyo pia alichangisha zaidi ya Shilingi
Milioni Tatu ambazo alidai kuwa zitasaidia wakati wa maandamano katika
kununulia maji ya kunawa baada ya kupigwa na mabomu pia kununulia dawa
za huduma ya kwanza kwa watakaoathirika na maandamano hayo.
|
No comments:
Post a Comment