TEKNOLOJIA waliyotumia
Google kutengeneza miwani ambayo ina uwezo wa kumpiga picha mtu au
kurekodi bila muhusika kujua (google glass) sio mpya ila Kampuni ya
Google ndio wakwanza kuja na teknoloji hiyo, ili kila mtu aweze kutumia
na inakadiriwa huwenda bidhaa hii ikafanya vizuri sana katika mauzo.
Google
glass ni rahisi sana kutumia, kama unataka kupiga picha unachotakiwa
kusema ni “OK Glass, take a picture.” upo kwenye foleni unaona fujo
unataka kuchukua video, mwambie Google Glass naye atakusaidia kuchukua
video. Hii ndio kali, unataka kuwaonyesha ndugu na marafiki kitu
unachokiona wakati huo huo? Google glass inafanya yote hayo, inakuja na
kitu kama “Skype-style video chat”.
Umesafiri
kwenda kuchukua mzigo China? Google glass itakusaidia kuchukua
kutafsiri lugha. Umeenda Zanzibar kutembelea majengo ya kitalii na
unabaki kushangaa shangaa, uliza Google glass na itakupa tour guide.
Google
glass ni kifaa ambacho unaweza kutumia kurekodi video, kupiga picha,
kutafuta habari katika Google, kutafsiri lugha, na unaweza fanya yote
haya bila kutumia mikono yako (hands free). Tatizo ni kwamba, ukishavaa
hiki kifaa kama miwani, watu hawajui kama unawarekodi kwenye video au
vipi, na kwa wabongo walivyo wanavyojua kujihami kupigwa picha au
kurekodiwa kwenye video, ukivaa Google glass unaweza tolewa baa.
Kwa
nchini Tanzania kifaa hiki ambacho kitakuwa na wastani wa bei ya sh.
mil 2. 2 ($1500). Hata hivyo kifaa hicho kinachovaliwa kama miwani,
sijui kama utaweza kutembea nacho hata hatua kumi kabla ya vibaka
kukuvaa baada ya kujua thamani yake. Tusubiri Google wakiwezeshe kifaa
hiki kiweze elewa kiswahili ndio na sisi tutakifaidi zaidi kwani hapa
hamna kubonyeza bonyesha ni kuongea tu. Je ukipata Google glass utatumia
kifaa hiki cha kisasa kufanyia nini? Acha maoni yako.
*Imeandaliwa na www.thehabari.com
No comments:
Post a Comment