Kutoka kushoto: Halima Mdee, Ester Bulaya na Neema Hamid.
WABUNGE
katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambao walihudhuria
mafunzo ya kijeshi katika kambi tofauti za Jeshi la Kujenga Taifa (JKT),
walipata msoto wa nguvu.
Kuonesha
jinsi ambavyo msoto ulikuwa wa nguvu, katika kambi ya Tanga, siku tu ya
utambulisho, mbunge wa Chadema (jina tunalo), alizimia.
Vilevile,
kwenye Kambi namba 832, Ruvu, Pwani, Mbunge wa Tarime, Nyambari
Nyangwine, alishindwa kuhimili kishindo cha depo, hivyo akatoroka, japo
mafunzo yenyewe yalikuwa ya muda wa wiki tatu tu.
Baadhi ya wabunge wakiwa katika pozi na wanajeshi wengine.
ILIKUWA KAZI KWELI
Siku ya kwanza tu ya kuripoti kambini, wabunge wote walipigwa vipara na baada ya hapo, ilifuata awamu ya kupima afya.
“Jeshi
ni jeshi tu, tulipimwa ukimwi bila hata kuandaliwa wala kupewa
ushauri,” alisema mmoja wa wabunge waliohudhuria depo hiyo (jina tunalo)
kisha akaongeza: “Mfano mimi ningeambiwa kule kuna kupima ukimwi hata
nisingeenda, nilikuwa sijapima kama miaka saba, dah kule ni hatari.”
Mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee, akinyolewa nywele.
KUHUSU VIPARA
Mbunge
mwingine alisema: “Walichotuweza ni ile tunaripoti tu, tunanyolewa
vipara halafu ndiyo taratibu nyingine zinafuata. Kama wangekuwa
wanatuonesha picha ya kile kitakachofanyika kabla ya kutunyoa, wengi
wetu tungetimka mapema.
“Tatizo
unanyolewa halafu ndiyo unapelekwa kupimwa ukimwi, sasa ukikataa kupima
na una kipara chako, mtaani utarudi vipi? Hata kunyoa, wengine tuliingia
na rasta, lakini wakatupiga upara wa wembe harakaharaka bila hata
kungoja kuzifumua.”
...Wakiwa mazoezini.
MAFUNZO YANA FAIDA?
Mbunge
wa Viti Maalum kwa tiketi ya Umoja wa Vijana wa CCM, Mkoa wa Mara,
Ester Bulaya, alisema kuwa anashukuru kupata mafunzo ya kijeshi, kwani
yamemjenga kwa kiasi kikubwa.
“Japo
ni kazi lakini tunatamani muda uongezwe, maana wiki tatu zilikuwa fupi,
program ni nyingi, kwa hiyo tukatakiwa kufanya kwa pamoja,” alisema
Bulaya kisha akaongeza: “Imenijenga kweli, najiona mkakamavu mwenye
uwezo zaidi wa kutumikia wananchi.”
Kwa
upande wa Mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee, alisema: “Natamani
kila mtu awe anapitia mafunzo ya JKT, maana siyo tu yanakujenga
kiukakamavu, bali pia yanakupa uzalendo na ari ya kuwatumikia wananchi.”
...Wakiwa katika picha ya pozi.
na global
No comments:
Post a Comment