Na.Mo
Blog Team.
Serikali
nchini imetakiwa kuacha kufanya mambo bila kutaka ushauri katika
masuala ya kuhama kutoka mfumo wa analojia kwenda digitalii na badala
yake ikae meza moja na wamiliki wa vyombo vya habari ili kupata muafaka
wa kweli na ikibidi ivipe ruzuku ili kuhakikisha uendeshaji wa vituo
hivyo katika mfumo huo mpya unafanikiwa.
Mwenyekiti
wa Chama cha NCCR Mageuzi Bw. James Mbatia (pichani), ameitaka
Serikali ikubali kwa nia njema kabisa angalau kwa muda wa miezi sita
ijayo au hata mwaka mzima ujao kwa mikoa mitatu, kutumia mfumo wa
analojia kwa kuwa ndio walikuwa wamejiandaa nao na ndio walikuwa
wamesajili nao vyombo hivi ili kujiandaa kuingia kwenye digitali.
Hata
hivyo serikali yenyewe imeshatoa tamko kwamba haitorudia nyuma kwenye
mfumo wa analojia na badala yake itaendelea kusonga mbele katika mfumo
wa digitali kwani tayari mfumo huo ni mfumo wa kiulimwengu.
Suala
hilo limeleta changamoto kubwa na wadau mbalimbali wa masuala haya ya
habari ambao wametaka kuwepo na mazungumzo ili kuweza kufikia muafaka
mzuri katika uendeshaji wa vyombo hivi vya habari kwa kuwa wenyewe
wanaona ni mzigo mkubwa kwa sasa kuingia katika mfumo huo wa digitali.
No comments:
Post a Comment