WAKATI
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kikionekana kutikiswa na ushawishi wa Waziri
Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa, wa kutaka kutimiza safari yake ya
kuwapatia Watanzania elimu bure, Mbunge wa Moshi Mjini, Philemon
Ndesamburo (CHADEMA), amejitokeza kumkingia kifua na kutaka asisakamwe.
Kauli ya Ndesamburo inakuja siku chache wakati kukiwa na harakati za
wazi wazi kuwapinga wanaotajwa kutaka kuwania urais, zikishika kasi
ndani ya CCM na kuonekana kuzigonganisha vichwa jumuiya zake.
Akitoa salamu zake za mwaka mpya jana, pamoja na kuzungumzia hali ya
kisiasa nchini kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu
mwakani, Ndesamburo alisema Lowassa hapaswi kushambuliwa kwa kigezo cha
kutangaza safari yake.
“Wanaotangaza nia mbona wako wengi sana huko CCM na wala siyo Lowassa
peke yake? Kwenye urais na hata huku chini kwenye ubunge na hata
udiwani wako wengi tu wanafanya hivyo. Ina maana hao wanaomnyooshea
kidole Lowassa hawa wengine hawawaoni?
“Hata huku kwenye vyama vyetu CHADEMA, CUF, NCCR-Mageuzi wapo
wanaotuvuruga, lakini sasa hivi habari ya mjini ni Lowassa, Lowassa…
kama kweli hatupendezwi na hali hiyo tuwanyooshee wote basi, kama
hatuwezi wamwache aendeleze ndoto yake. The best way to predict the
future is to invent it,” aliongeza Ndesamburo.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz
Alisema kwa mantiki hiyo, njia sahihi aliyoitumia Lowassa ya kutamka
hadharani kusudio la kukamilisha majaliwa ya ndoto zake, ni namna
alivyonyambulisha kile kinachoshabihi mawazo yake ya muda mrefu ya
kuwatumikia Watanzania wenzake.
Ndesamburo ambaye pia ni Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Kilimanjaro,
alisema haijalishi kwamba yeye ni mpinzani wa CCM, lakini kumshambulia
Lowassa peke yake, ingali kuna vinara wengine wanaokigawa chama chao si
haki.
“Haijalishi ya kuwa mimi ni mpinzani na najua hata wao wanalijua hilo
kwamba Ndesamburo ni nguli wa siasa za mageuzi ya kifikra katika
taifa, nasema wawatizame na hao wengine wanaopita huko huko makanisani
na misikitini kujitangaza kwa kisingizio cha kualikwa katika harambee,”
alisema Ndesamburo.
Hata hivyo, Ndesamburo amewaomba Watanzania kuwachagua wagombea wa
CHADEMA watakaopitishwa kupeperusha bendera ya chama hicho katika
uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu kwa kuwataka kuwakataa watu
wanaotaka kuwachagulia viongozi wa kuwaongoza.
Katika siku za karibuni kumekuwa na matamko ya makatazo kutoka kwa
viongozi wa CCM wakiwemo wale wa jumuiya, yakimtaka waziri huyo mstaafu
kuacha kuendelea na kile kinachodaiwa kuwa kampeni za chini kwa chini za
kuusaka urais.
TANZANIA DAIMA
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz
No comments:
Post a Comment