Rais wa
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi akizungumza
kwenye uzinduzi wa programu ya Ishi Huru jijini Dar es Salaam.
Rais wa
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amezindua
programu ya kutoa elimu ya kupambana na matumizi ya dawa za kulevya kwa
vijana iitwayo Ishi Huru.
Programu hiyo iliyozimduliwa tarehe 10
Januari mwaka huu jijini Dar es Salaam iko chini ya taasisi ya Africa
Inside Out inayoongozwa na Rebecca Young wakati washirika (partners) ni
TFF na kampuni ya Rhino Resources ya Marekani.
Rais Malinzi amesema matumizi ya dawa
za kulevya nchini yamekuwa yakiongezeka, hivyo kuwa kikwazo kwa
maendeleo ya vijana ambapo ameipongeza Africa Inside Out kwa programu
hiyo kwa vile itazuia vijana wengi kujiingiza katika matumizi ya dawa
hizo.
"Moja athari kubwa za matumizi ya dawa
za kulevya ni kupata maambukizi ya virusi vya Ukimwi kutokana na
kuchangia sindano za kujidunga dawa hizo.
"TFF tutatoa ushirikiano wa kutosha
katika programu hii. Lakini pia tutaingiza Ishi Huru katika programu
zetu za mpira wa miguu kwa vijana. Tutahamasisha jamii katika kupambana
na dawa za kulevya," amesema.
Katika uzinduzi huo, pia Rais Malinzi
alizundua semina ya waelimishaji na kuwaeleza kuwa wamepata fursa hiyo
kwa vile ni vijana wanaojituma, hivyo watafikisha vizuri ujumbe wa Ishi
Huru katika shule na vituo vya vijana nchini.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz
No comments:
Post a Comment