Mjumbe
wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete
akiwasili eneo la mkutano wa hadhara, uliofanyika Kata ya Ndoro, Lindi
mjini, Feb 20, 2013.
Kina
Mama wa Kata ya Ndoro Lindi Mjini, Amina Ali na Saida Ali wakimzawadia
kuku, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete,
wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika, Februari 20, 2013 katika kata
hiyo.
Baadhi ya wananchi
waliohudhuria mkutano wa hadhara wa Mama Salma Kikwete, Kata ya Ndoro,
Lindi mjini wakishangilia wakati wa mkutano huo.
Wasanii
Karim Suleiman ambaye ni mlemavu wa mguu na Mohamed Ali wakionyesha
umahiri wao wa kucheza Kiduku katika mkutano wa hadhara uliofanywa na
Mama Salma Kikwete kwenye Kata ya Ndoro, Lindi mjini Februari 20, 2013.
Wanachama
wapya wa CCM wakila kiapo baada ya Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM,
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete kuwakabidhi kadi wanachama wapya katika
mkutano wa hadhara uliofanyika mtaa wa Matopeni, Lindi mjini Feb 20,
2013. (Picha zote na Bashir Nkoromo).
Na
Anna Nkinda, Maelezo Lindi
Mjumbe
wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (NEC), Mama Salma
Kikwete amewataka wakazi wa wilaya ya Lindi mjini kujenga mazoea ya
kwenda hospitali kupima afya zao mara kwa mara na kuachana na tabia ya
kwenda kutibiwa kwa waganga wa jadi na kushikana uchawi kutokana na
maradhi yanayowasumbua.
Mama
Kikwete ambaye pia ni Mke wa Rais alitoa rai hiyo jana alipokuwa
akiongea kwa nyakati tofauti na wakazi wa kata za Matopeni na Wailesi
zilizopo wilaya ya Lindi mjini wakati wa ziara yake ya kichama ya siku
saba katika wilaya ya Lindi mjini ya kuwashukuru wanachama wa CCM kwa
kumchagua kuwa mjumbe wa NEC.
Aliwasihi
watu wenye tabia ya kutopenda kupima afya zao wakati wanaumwa na wale
wenye tabia za kukimbilia kwa waganga wa jadi huku wakijua fika kuwa ni
wagonjwa waache kwani wanaweza kupoteza maisha kwa magonjwa ambayo
wangeweza kutibiwa katika vituo vya afya na kupona.
“Hakuna
mtu asiyejua kuwa kuna Ugonjwa wa Ukimwi, muache suala la kushikana
uchawi katika hili kwani ugonjwa huu haupatikani kwa kurogwa. Mtu mwenye
virusi vya ukimwi anapimwa kinga za mwili za kupambana na magonjwa (
CD4) kama zipo chini atapewa dawa za kuongeza na akitumia dawa atakuwa
na nguvu na kuweza kufanya kazi zake kama zamani jambo la muhimu
asipitishe muda wa kuzitumia” , alisema Mama Kikwete.
Aidha
Mjumbe huyo wa NEC alisema kuwa jamii nzima inahusika katika ulezi wa
watoto lakini jambo la kusikitisha ni kuwa hivi sasa watu wamebadilisha
mienendo ya maisha kila mtu anahangaika kulea mwanawe. Na kuwasihi
wakazi wa Lindi kufuata maadili ya zamani ya kuwalea watoto kwani
mtoto wa mwenzako ni wako .
“Ni
jukumu la jamii nzima kuwalea watoto wao kwa kufuata mila za
kitanzania , wazazi ambao wakiambiwa kuwa watoto wao wanamienondo mibaya
na kuja juu badala ya kuzifanyia kazi taarifa hizo waache tabia hiyo
kwani watoto wakilelewa vizuri hata shuleni watakuwa na maadili mazuri
na kuweza kufanya vizuri katika masomo yao”, alisema.
Kuhusu
ufanyaji kazi kwa ushirikiano Mama Kikwete aliwataka wananchi hao
kuachana na mambo ya siasa kwani uchaguzi umeshapita hivyo basi wafanye
kazi za maendeleo kwa na kujenga tabia ya kujitolea kufanya kazi.
Mama
Kikwete alihoji, “Hawa wazungu manaowaona wanakuja Lindi kufanya kazi
wamekuja kujitolea ni jambo la muhimu kujitolea kufanya kazi za
maendeleo, ukiambiwa kuna ujenzi wa shule, Zahanati wewe nenda
ukajitolee usiseme ile si kazi ya Serikali sasa Serikali ni nani kama si
wewe mwananchi?”.
Akisoma
taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi 2010 – 2015 Diwani wa kata
ya Matopeni Suleiman Namkoma alisema kuwa idadi ya watoto wanaoanza
darasa la kwanza imeongezeka kutoka 45 hadi 60, kuongezeka kwa ufaulu wa
wanafunzi wanaofanya mtihani wa darasa la saba kutoka 20 hadi 43,
kuongezeka kwa barabara zinazopitika kipindi cha masika na kiangazi na
kuimarika kwa miundombinu na barabara za mifereji.
Namkoma
alisema, “Tunakabiliwa na changamoto za uchache wa wataalam wa kada
mbalimbali ngazi ya kata na jamii kukosa wataaluma wa huduma stahiki,
ukosefu wa uwajibikaji kwa baadhi ya watumishi wa ngazi ya kata, ukosefu
wa huduma ya maji safi na salama, kuchelewa kwa ruzuku ya Serikali kuu
na makusanyo madogo ya Halmashauri na upungufu wa walimu wa shule ya
msingi”.
Kwa
upande wake Diwani wa kata ya Mikumbi Zahara Suleiman alisema kuwa
katika kata hiyo kuna vikundi vingi vya maendeleo lakini kwa mwaka
2010/2013 hakuna vikundi vilivyokopeshwa na Seambavyo ni Ayayoli na
Mafundi Seremali.
Suleiman
alisema, “Tunawashukuru wafadhili waliovikopeshwa baadhi ya vikundi
vyetu vya maendeleo kwani kikundi cha Mwambao Fishing Group kilipewa na
Mama Salma Kikwete boti na vifaa vya kuvulia vyenye thamani ya shilini
milioni 57 na kikundi cha Uganda kilipewa pesa kutoka MACEP shilingi
milioni 15”.
Katika
mkutano wa kata ya Mikumbi Mjumbe huyo wa NEC aliwapokea vijana 18
waliokuwa wanachama wa CUF na kujiunga na CCM. Akiwa katika kata za
Matopeni, Wailesi na Mikumbi alikabidhi kadi kwa wanachama wapya wa
CCM 43 , Umoja wa vijana 60, Umoja wa Wanawake 22 na Jumuia ya Wazazi
59.
No comments:
Post a Comment