Mgeni Rasmi katika Kongamano la
Nane la Wanahabari na Wadau wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya
(NHIF), Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii,Dkt. Seif Rashid (kulia)
akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara,Mh. Joseph Simbakalia (katikati)
pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Mtwara,Mh. Wilman Kapenjama
Ndile (kushoto) wakiwasili kwenye Ukumbi wa Benjamin Mkapa uliopo ndani
ya Chuo cha Ualimu Mkoani Mtwara leo,tayari kwa ufunguzi wa Kongamano
hilo ambalo ni la siku mbili.
Mwenyekiti wa Kongamano la Nane la
Wanahabari na Wadau wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF),John Bwire
akitoa utambuliwa wa Wanahabari waliohudhulia kongamano hilo toka
sehemu mbali mbali hapa nchini,linaloendelea kufanyika hivi sasa kwenye
Ukumbi wa Benjamin Mkapa uliopo ndani ya Chuo cha Ualimu Mkoani Mtwara.
Mgeni Rasmi katika Kongamano la
Nane la Wanahabari na Wadau wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya
(NHIF),Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii,Dkt. Seif Rashid akitoa
hotuba yake ya ufunguzi wa Kongamano hilo linalofanyika hivi sasa kwenye
Ukumbi wa Benjamin Mkapa uliopo ndani ya Chuo cha Ualimu Mkoani
Mtwara.Kauli mbiu ya Kongamano hilo kwa mwaka huu ni “Matumizi Sahihi ya
Fedha za Uchangiaji Katika Halmashauri ili kuboresha huduma katika
vituo vya matibabu”.
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara,Mh. Joseph
Simbakalia akizungumza machache kabla ya kumkaribisha mgeni Rasmi
kuhutubia na kufungua Kongamano hilo.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya ambaye ni
Mwenyekiti wa Wakuu wa Mikoa yote Nchini,Mh. Abbas Kandoro akitoa salamu
kwa Wanahabari na Wadau wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF)
wanaoshiriki Kongamano hilo.
No comments:
Post a Comment