KASI
ya kuzuia ukwepaji kodi za Serikali uliofanywa kwa kipindi cha miezi mitatu na
utawala wa Rais Dk. John Magufuli kwa ‘kutumbua majipu’ umeokoa wastani wa Sh
bilioni 700.
Katika
utawala wa Serikali iliyopita ya awamu ya nne, wastani wa makusanyo ya kodi kwa
kiwango cha juu kwa mwezi yalikuwa Sh bilioni 900, lakini baada ya kuingia kwa
awamu hii kumekuwapo na ongezeko la zaidi ya Sh bilioni 700 kwa miezi mitatu ya
Desemba hadi Februari.
Akitangaza
ongezeko hilo kwa waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Kaimu Kamishna Mkuu
wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Alphayo Kidata, alisema katika kipindi cha
Desemba 2015, pia TRA iliweza kuvuka lengo kwa kukusanya kiasi cha zaidi ya Sh.
trilioni 1.4 sawa na ongezeko la wastani wa Sh. bilioni 490 kwa mwezi.
Alisema
kiasi hicho ni kikubwa kikilinganishwa na wastani wa makusanyo kwa mwezi Julai
hadi Novemba mwaka jana ambapo ilikuwa ni Sh. bilioni 900 kwa mwezi. Like page
yetu ya facebook Jambo Tz
Kidata
alisema katika mkakati wa Serikali ya awamu ya tano ya Rais Magufuli ya
kuhakikisha mapato ya nchi hayapotei TRA imefanikiwa kukusanya kiasi cha Sh.
trilioni 8.5 kwa kipindi cha mwezi Julai mwaka jana hadi Februari, makusanyo
ambayo ni sawa na asilimia 99 ikilinganishwa na lengo la Sh. trilioni 8.6.
Kwa
mujibu wa Kidata, TRA imejiwekea mikakati mizuri ikiwa ni pamoja na kuziba
mianya ya upotevu wa mapato bandarini mwezi Februari, ambapo kwa upande wa
Tanzania Bara na Zanzibar walifanikiwa kukusanya kiasi cha Sh. trilioni 1.04
ambazo ni sawa na asilimia 101.18 ya lengo la Sh. trilioni 1.02.
Alisema
katika kipindi cha mwezi Januari kwa upande wa Tanzania Bara na Zanzibar
walikusanya Sh. trilioni 1.07 ambazo ni sawa na asilimia 102 ya lengo la Sh.
trilioni 1.05. Like page yetu ya facebook Jambo Tz
Katika
kipindi cha mwezi Desemba 2015, pia TRA iliweza kuvuka lengo kwa kukusanya
kiasi cha zaidi ya Sh trilioni 1.4, mapato ambayo ni sawa na ongezeko la
wastani wa Sh. bilioni 490 kwa mwezi ukilinganisha na wastani wa makusanyo kwa
mwezi Julai hadi Novemba ambayo yalikuwa Sh. bilioni 900.
“Makusanyo
hayo yametokana na uthubutu ambao TRA imejiwekea katika kusimamia na
kuhakikisha inaendelea kuziba mianya ya ukwepaji wa kodi na kuweka mazingira
rafiki kwa mlipakodi kulipa kwa wakati na urahisi kwa kutumia mifumo mbalimbali
iliyopo,” alisema Kidata.
Alisema
wameweka mikakati katika ukusanyaji wa kodi kwa kipindi cha mwezi Machi hadi
Juni kuhakikisha kwamba wanaendelea kudhibiti mianya ya ukwepaji wa kodi,
kufichua wakwepa kodi, kupambana na rushwa na kuongeza wigo wa kodi kwa
kusajili wafanyabiashara ambao hawajasajiliwa.
Pia
kusimamia kwa karibu matumizi ya mashine za EFDs na utoaji wa risiti,
kufuatilia na kudai malimbikizo ya kodi kutoka kwa wadaiwa sugu, kuendelea na
ukaguzi wa kodi kwa wafanyabiashara ikiwa ni pamoja na maofisa wa TRA na
kutekeleza majukumu yao kwa weledi na uadilifu.
Katika
hatua nyingine, Kidata alisema mamlaka hiyo imefuta bei elekezi kwa bidhaa
zinazoingizwa nchini kutokana na kuwa ipo kinyume na sheria, huku ikilenga
kutengeneza mazingira mazuri kwa wafanyabiashara ili haki itendeke katika suala
zima la ulipaji wa kodi. Like page yetu ya facebook Jambo Tz
No comments:
Post a Comment