Jeshi nchini Nigeria linasema
kuwa linajua wanakozuiliwa zaidi ya wasichana 200 waliotekwa nyara
majuma sita yaliyopita lakini likasema haliwezi kutumia nguvu
kuwakomboa.
Afisa wa cheo cha juu jeshini - Mkuu wa Jeshi
Alex Badeh - aliwambia waandamanaji jijini Abuja kuwa hangeweza kufichua
waliko wasichana hao lakini akaahidi kuwa wanajeshi watawarejesha
nyumbani wasichana hao.Alisema anaamini kuwa watawarudisha wasichana hao nyumbani hivi karibuni lakini akaeleza masikitiko yake kwa kile alichosema watu kutoka nje ya nchi wanaochochea ghasia na maandamano.
Bwana Badeh alisisitiza kuw kutumia nguvu kujaribu kuwakomboa wasichana hao ni hatari.
"Wapiganaji hawa wanataka kupigana na kwa hivyo wasichana watakuwa hatarini ikiwa kutatokea mkabiliano makali kati ya wapiganaji hao na jeshi la Nigeria," Alex Badeh alisema. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz
Na BBC Swahili
No comments:
Post a Comment