Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison
Mwakyembe jana usiku alikuwa katika wakati mgumu wakati Bunge lilipoketi
kama Kamati ya Matumizi, kiasi cha kutishia bajeti ya wizara yake
kukwama. Hata hivyo, Makadirio ya Mapato na Matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2014/15 yalipitishwa.
Wabunge wa vyama vyote walimbana Dk Mwakyembe na
kutoa shilingi karibu katika kila kifungu wakihoji mambo mbalimbali hasa
juu ya mgogoro wa umiliki wa Shirika la Usafiri Dar es Salaam (Uda),
uimarishaji wa Shirika la Ndege Tanzania (ATC), usafiri wa majini
hususan usalama wa meli ya Mv Victoria.
Sakata la Uda
Sakata hilo la Uda lilisababisha mvutano baina ya
Naibu Spika, Job Ndugai na Dk Mwakyembe ambaye alilalamikia mjadala wa
Uda kuruhusiwa katika hotuba ya wizara yake. Hata hivyo, Ndugai alipangua hoja hiyo akisema
mbali na kwamba Uda inagusa wizara nyingi, lakini ni suala linalohusu
uchukuzi hivyo ilikuwa sahihi kujadiliwa katika mjadala huo.
Mbunge wa Nzega (CCM), Dk Hamisi Kigwangalla ndiye
aliyeibua suala hilo kwa kuhoji sababu ya Serikali kutoa taarifa
zinazokanganya kuhusu Uda, hali kamati anayoiongoza ilishakaa na pande
zote husika wakiwamo wataalamu na kuwa na hitimisho kwamba Kampuni ya
Simon Group Ltd ni waendeshaji halali wa shirika hilo. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz
Hoja hiyo iliibua mjadala ambao pia ulichangiwa na
Mwenyekiti wa Kamati ya Miundombinu, Peter Serukamba ambaye alisema
Simon Group Ltd waliuziwa kihalali hisa za Uda na kwamba wamiliki hao
wanazongwa kutokana na kwamba ni ngozi nyeusi (Watanzania).
Kwa upande wake, Waziri Kivuli wa Uchukuzi, Moses
Machali alisema maelezo ya Serikali kuhusu umiliki wa Uda yana
mkanganyiko, hivyo Simon Group Ltd wanaandamwa bila sababu za msingi. Kwa upande wake Kiongozi wa Upinzani Bungeni,
Freeman Mbowe alisema Serikali inajiweka uchi, kutokana na majibu
yanayokinzana kutoka kwa mawaziri na Kamati za Bunge.
Hoja ya Mbowe ilipingwa na waziri wa Nchi, Ofisi
ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), aliyesema Serikali haijajivua
nguo na kwamba itachukua hatua za kuliweka sawa kwa kutoa taarifa moja. Awali, akihitimisha hotuba yake huku akipangua
hoja mbalimbali za wabunge, Dk Mwakyembe alisema mwaka 2012/2013 ilikuwa
ni kuitoa Sekta ya Uchukuzi kutoka katika chumba cha wagonjwa mahututi.
Na Waandishi Wetu, Mwananchi
Mapema akisoma hotuba ya Kambi Rasmi ya Upinzani, Machali
alisema Mei 15 mwaka huu, Naibu Waziri wa Fedha, Adam Malima aliliambia
Bunge kuwa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ilikuwa na hisa asilimia
51 na Serikali 49. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz
Alisema mara baada ya kutolewa taarifa hiyo,
Mkurugenzi wa Simon Group, Robert Kisena alidai kuwa kampuni hiyo
inamiliki asilimia 76.79 na Serikali asimilia 23.26 tu.
“Je, ni nani mwongo kati ya Serikali na Simon
Group? Je, aliye mwongo kati yao ndani na nje ya Bunge anachukuliwa
hatua gani?” alihoji.
Masuala mengine ambayo yaliibua mjadala wakati
Bunge lilipokaa kama Kamati ya Matumizi ni kuhusu Shirika la Ndege la
ATCL, Upanuzi wa Viwanja vya Ndege vya Mwanza na Kilimanjaro (Kia) na
usalama wa Meli ya Mv Victoria.
Majibu ya Dk Mwakyembe
Akijibu hoja hizo, Dk Mwakyembe alisema bajeti ya
mwaka huu wa fedha 2014/2015 ni ya kuiendeleza sekta ya uchukuzi ili
iweze kukimbia. “Mwaka 2013/2014 ilikuwa ni bajeti ya kuifanya
sekta hii ya uchukuzi ianze kutembea. Nawahakikishia mwaka wa fedha wa
2014/2015 kutakuwa na mabadiliko makubwa katika sekta ya reli itaanza
kukimbia,” alisema.
Alisema kwa mara ya kwanza nchi itakuwa na vichwa
vya treni 51 vya uhakika tofauti na idadi ya sasa ambayo ni vichwa
vinane tu vya kusuasua na kwamba kwa kuwa na vichwa hivyo kutawezesha
kusafirisha tani milioni 1.5 za mizigo kulinganisha na tani 200,000 za
sasa.
Kuhusu wabunge, mawaziri na wafanyakazi wa Mamlaka
ya Bandari Tanzania (TPA), kutumia fedha nyingi kwa ajili ya safari, Dk
Mwakyembe alisema taarifa hiyo si sahihi na kwamba hakuwahi kufanya
safari yoyote ya mafunzo kwa sababu taaluma yake. Kwa upande wa ATCL, Dk. Mwakyembe alisema deni la Sh133 bilioni ndilo linalowasumbua na kwamba Serikali inahangaika kulichukua.
Awali, Kambi rasmi ya upinzani Bungeni, iliilipua
Wizara ya Uchukuzi kwa kile ilichodai ufisadi na matumizi mabaya ya
madaraka ikiwemo kuhoji hatua ya wizara hiyo kujitengea Sh1.1 bilioni
kwa ajili ya kulipana posho na chai. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz
Na Waandishi Wetu, Mwananchi
No comments:
Post a Comment