Al Shabaab wamesema katika
taarifa kuwa kwa kushambulia mgahawa huo, walikuwa wakiwalenga raia wa
mataifa ya Magharibi wanaopendelea kuutembelea Djibouti.
Kundi hilo liliwalaumu Wafaransa - walio na
kambi kubwa ya wanajeshi nchini Djibouti - kwa kuwadhulumu Waislamu
katika Jamhuri ya Africa ya Kati (CAR) na kwa kutoa mafunzo kwa
wanajeshi wa Djibouti walio katika kikosi maalumu cha wanajeshi wa Umoja
wa Afrika, AMISON, nchini Somalia.Al Shabaab wamepunguzwa makali nchini Somalia tangu kuanzishwa kwa msukumo wa kijeshi wa kukabiliana nao wa Serikali ya Somalia na wanajeshi wa AMISOM.
Hata hivyo kundi hilo halijaishiwa na uwezo wa kushambulia. Mnamo Jumanne wanajeshi kadhaa wa Ethiopia waliuawa baada ya kuvamiwa na Al Shabaab katika eneo la Bakol.
Na Jumamosi, walishambulia Bunge katika mji mkuu wa Mogadishu.
Kwa kuwa kundi hilo tayari linaweza kushambulia nchini Kenya na sasa limechipukia Djibouti, ni ishara kamili kuwa limeanza kuwa tatizo katika eneo zima, mbali na kushambulia taasisi mbalimbali nchini Somalia. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz
Na BBC Swahili
No comments:
Post a Comment