Malumbano
makali ya maneno na hoja yamezuka baina ya Kiongozi wa Kanisa Katoliki
duniani, Papa Francis na Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu
kuhusu lugha gani aliyotumia Yesu Krtisto miaka 2,000 iliyopita.
Viongozi hao Jumatatu mchana wakati wa ziara ya
siku tatu ya Papa aliyoifanya katika eneo la Mashariki ya Kati ikiwa ni
ziara yake ya kwanza tangu atwae wadhifa huo. “Yesu aliishi hapa katika
ardhi ya nchi hii. Alizungumzia Kiebrania,” alianza Netanyahu wakati
akimweleza Papa Francis kwenye mkutano wa hadhara mjini Yerusalemu.
Netanyahu, pia akaeleza kuwa upo uhusiano wa karibu baina ya mahali alikozaliwa Yesu na Ukristo. Naye Papa Francis akasikiliza kwa muda, kisha akajibu: “Yesu alizungumza lugha ya Kiaramaiki.”
“Ndiyo, nimesema alizungumza Kiaramaiki, lakini pia alijua Kiebrania,” akaingilia kati Netanyahu.
Hata hivyo, mjadala huo umepokewa kwa hisia
tofauti na watu wengi ambao wamekuwa wakifuatilia ziara ya siku tatu ya
Papa Francis katika nchi takatifu. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz
Mtaalamu wa masuala ya lugha, raia wa Israel,
Profesa Ghil’ad Zuckermann ameliambia Shirika la Habari la Reuters
kwamba wawili hao, Netanyahu, ambaye ni mtoto wa mtaalamu wa historia ya
Kiyahudi na Papa Francis, kiongozi wa kiroho anayeongoza waumini
bilioni 1.2 Wakatoliki, kila mmoja ana hoja. “Yesu alikuwa mzungumzaji
wa Kiaramaiki,” anasema Profesa Zuckerman kuhusu lugha hiyo ambayo
imetoweka yenye uhusiano na Kiebrania. “Pia, anaweza kuwa alizungumza na
kufahamu Kiebrania, lugha ambayo ilitumika kwenye maandiko.”
Prof Zuckermann alisema kuwa wakati wa Yesu,
Kiebrania kilizungumzwa na watu wa madaraja ya chini - “ambao ndiyo
aliowahubiria”. Mojawapo ya vitu vingi katika eneo la Mashariki ya Kati
hadi sasa ni kuhusu utata wa Yesu, utata huo umechukua pia sura na
mtazamo wa kisiasa.
Yesu, Myahudi alizaliwa kwenye mji wa Bethlehemu
ambao ulikuwa chini ya himaya ya Warumi, kwenye Mkoa wa Yudea, katika
ardhi inayoshikiliwa kwa sasa na Israel kwenye Ukanda wa Magharibi.
Alikulia mjini Nazareth , akaendesha utume kwenye
mji mwingine wa Galilea, ambao pia uko kaskazini mwa Israel, alifia
mjini Yerusalemu, mji ambao unatukuzwa na Wayahudi, Wakristo na
Waislamu, ambao unagombewa na tawala za Israel na Palestina hadi sasa.
Kwa upande wao, Wapalestina wamekuwa wakidai kuwa
Yesu ni Mpalestina. Hata hivyo, utawala wa Israel umekuwa ukipingana na
mtazamo huo.Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz
No comments:
Post a Comment