Raia wa Misri wanapiga kura kwa
muda wa siku mbili kumchagua rais mpya chini ya ulinzi mkali kuhakikisha
mchakato wa upigaji kura unafanyika kwa usalama.
Karibu maafisa wa usalama laki mbili wameshika
doria kote nchini Misri serikali ikionya dhidi ya hatari za usalama
zinazoweza kusababishwa na itikadi kali za kiislam .Oparesheni kubwa ya usalama inayoendelea nchini Misri ni ushahidi kamili kuwa utawala wa sasa unaoungwa mkono na jeshi unatambua kuwa ugaidi unaoungwa mkono na Waislamu wenye itikadi kali upo na unaweza kuteguliwa wakati wo wote.
Mbinu ya kukabiliana na ugaidi huo ya Abdel Fatah al-Sisi haijabadilika ila tu ni magwanda yake ya kijeshi ya field Mashel yaliyojaa medali yaliyobadilishwa na nguo za kiraia.
Ametangaza katika kampeni yake kuwa anaunga mkono kuangamizwa kabisa kwa kundi la Muslim Brotherhood ambalo limeshuhudia maelfu ya wanachama wake wakizuiliwa na mamia wakihukumiwa vifo.
Bwana Sisi ametoa wito kwa watu wanaotakia Misri amani na utangamano baada ya miaka kadhaa ya mapinduzi na ghasia na ameheshimiwa kiwango cha kusujudiwa na wengine hivi kwamba unaweza kununua peremende au chokoleti dukani iliyopachikwa picha yake.
Mpinzani wake mwenye mrengo wa kushoto, Hamdeen Sabbahi, anatajwa katika vyombo vya habari ambavyo vinaoenekana kuamua tayari kuwa yeye atashindwa katika Uchaguzi unaoanza leo.
Ingawa wapiga kura wana mazoea ya kubadilika dakika za mwisho kabla ya uchaguzi lakini wengi nchini Misri watashangaa iwapo Bwana Sisi hashindi uchaguzi huu, na tena kwa urahisi. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz
Chanzo: BBC
No comments:
Post a Comment