Kamati ya Umoja wa Mataifa
dhidi mateso imelaumu vikali kanisa Catholiki kwa kutoshughulikia
ipasavyo suala la unyanyasaji wa ngono ndani ya kanisa hilo.
Katika ripoti iliyochapishwa hivi karibuni na
Umoja huo mjini Geneva , Kamati hiyo imeushutumu utawala wa Vatican kwa
kuwahamisha watawa kutoka parokia moja hadi nyingine kuwaepusha
kushtakiwa, na kupuuza haki za waathiriwa za kupokea fidia .Kamati hiyo imekasirishwa zaidi na kwamba Utawala wa Vatcan unasisitiza kuwa unahusika zaidi na wahudumu wanaofanyika kazi ndani ya Vatcan kwenyewe , kuliko makasisi wake wanaofanyika kazi kwingineko duniani.
Mwezi Januari mwaka huu utawala wa Vatican ulichunguzwa upya na kamati ya Umoja wa Mataifa kuhusu haki za watoto, baada ya kupokea ukosoaji kama huo kwamba ulishindwa kuwalinda watoto waliokuwa chini ya uangalizi wake. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz
Chanzo: BBC
No comments:
Post a Comment