Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
WAWAKILISHI wa Tanzania katika michuano mipya ya CECAFA Nile
Basin Cup inayoendelea nchini Sudan , Mbeya City fc wanaanza kutupa
karata yao ya kwanza leo hii majira ya 11:30 jioni kwa saa za Sudan
dhidi ya Academie Tchite ya Burundi.
Kuelekea katika mechi hii itakayopigwa uwanja wa Al-Merreikh
mjini Khartoum, ushinidi ni muhimu kwa Mbeya City fc ili kupata morali
ya mashindano haya yaliyoanza jana kwa mechi tatu kupigwa viwanja viwili
tofauti.
Kocha Juma Mwabusi ameuambia mtandao huu kwa njia ya simu kutoka
nchini Sudan kuwa kikosi chake kipo salama na kipo tayari kwa ajili ya
mechi ya leo jioni.
“Tumewasili salama mjini Khartoum. Tulichelewa kufika huku ili
angalau kuzoa hali ya hewa. Lakini haimaanishi hatuwezi kushindana. Sisi
tumejiandaa vizuri na tulikaa Dar kwenye joto ingawa hailingani na
Sudan”.
“Mashabiki wetu wawe na imani na timu yao. Tunaiwakilisha nchi
na tutapambana kwa nguvu zote. Wachezaji wana morali ya kufanya vizuri”.
Alisema Mwambusi.
Mbali na mchezo huo wa jioni, mechi nyingine ya usiku itakuwa baina ya AFC Leopard ya Kenya dhidi ya Enticelles ya Rwanda.
Katika mechi zilizopigwa jana, kwa mujibu wa msemaji wa CECAFA
Rodgers Mulindwa, Victoria University ya Kenya iliilaza Malakia FC ya
Sudan kusini bao 1-0.
Wenyeji Al-Merreikh waliibuka na ushindi mnono wa mabao 3-0 dhidi ya Polisi ya visiwani Zanzibar.
Nao Al-Shandi waliibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Dkhill ya Djibouti. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz
No comments:
Post a Comment