Saturday, May 24, 2014

CCM: "HATUWEZI KUWAVUMILIA WATENDAJI WA SERIKALI WANAOKWAMISHA UTEKELEZWAJI WA ILANI YA CHAMA CHA MAPINDUZI"

Katibu wa CCM wilaya ya kilolo Bw. Raphel Mahumba mwenye pama, akimuagiza Diwani wa kata ya ukumbi afuatilie nani anaye kwamisha ujenzi wa zahanati ya kitowo na hatua zichukuliwe haraka, aliye vaa skafu ni katibu mwenezi wa chama.
Wananchi waliongozana na katibu wa CCm wilaya ya Kilolo kuangalia ujenzi wa zahanati ya Kotowo ambayo imesimama bila sababu za msingi. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz
http://jambotz8.blogspot.com/
Katibu wa CCM wilaya ya Kilolo Bw. Raphael Mahumba akikagua mradi wa zahanati ambao umesimama bila sababu za msingi.
Katibu wa CCM wilaya ya Kilolo Bw. Raphael Mahumba akikagua mradi wa zahanati ambao umesimama bila sababu za msingi.
Wanakijiji wakitoka kuangalia sehemu ambapo ujenzi wa zahanati umesimama bila sababu za msingi katika kijiji cha Kitowo.
Katibu wa CCM wilaya ya Kilolo na katibu mwenezi wa chama wakisikiliza jambo kutoka kwa mwanakijiji.

Wananchi wakisikiliza kwa umakini mkubwa.
Mtendaji wa kijiji cha Masarali akijibu malalamiko ya wanakijiji mbele ya katibu wa CCM wilaya ya Kilolo.
Baadhi ya wanakijiji waliojitokeza kuhudhuria mkutano wakibadilishana mawazo.
Maneno hayo yamesemwa na katibu wa CCM wilaya ya Kilolo katika ziara yake inayoendelea katika wilaya ya kilolo akiwahutubia wanakijiji wa kijiji cha Kitowo na Masarali katika kata ya Ukumbi, katika ziara hiyo aliongozana na katibu mwenezi wa chama na katibu wa wazazi wilaya.
 Katibu huyo wa CCM ambaye ameonekana kuwa mtendaji mzuri wa kazi kuliko maneno amewahakikishia wanakijiji hao kuwa hawatawavumilia watendaji ambao wanasababisha shughuri za kimaendeleo zisifanyike kwa maslahi yao hivyo kupelekea wananchi kukichukia chama cha mapinduzi kwa ajiri ya watu wachache, aidha katibu huyo amemwagiza diwani wa kata ya Ukumbi kuwa ahakikishe ndani ya mwezi mmoja maji yanatoka katika kijiji cha Kitowo.
Pia katika ziara hiyo katibu ametoa msimamo wa chama cha mapinduzi wa kuunga mkono serikali mbili na akitoa sababu kuwa serikali tatu ni kuwaongezea mzingo wananchi ambao kodi zao ndio zitategemewa kuendesha serikali ya Tatu hivyo amewataka wananchi kuwapuuza watu wanao taka serikali tatu kwani hawaitakii mema nchi yetu. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz
Imeandikwa Na Kayanda Manyanya

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...