Tangu mwaka 2012 zaidi ya watoto 154 wamezaliwa
na wanawake walio juu ya umri wa miaka 50. Miongoni mwao, wamo
waliotokana na teknolojia ya upandikizaji. Pamoja na madaktari kuonya kuwa kuzaa katika umri
mkubwa kunahatarisha maisha ya mama na mtoto, wanawake hasa matajiri
wamekuwa wakizaa katika umri mkubwa. Wilayani Handeni Mkoa wa Tanga,
Mwajuma Seif (50) aliweka rekodi ya kujifungua watoto mapacha katika
umri huo.
Lakini Mwajuma ana kingine cha ziada tofauti na
wanawake wengi wanaozaa katika umri huo; alizaa kwa njia ya kawaida na
si kwa teknolojia ya upandikizaji. Tofauti nyingine ya mwanamke huyo si kwamba alizaa katika umri huo kwa kuwa hakuwa na mtoto; ujauzito huo ulikuwa ni wa 13. Daktari anayemwangalia Mwajuma, Elinisa Mushi
anasimulia mkasa wa mwanamke huyo akisema pamoja na umri, kingine
kilichomshangaza ni mtoto wa ajabu aliyemzaa .
Anaeleza kuwa walimpokea Mwajuma, ambaye ni mkazi
wa Kata ya Sindeni zaidi ya mwezi mmoja uliopita akiwa na ujauzito,
lakini walishangazwa na tumbo la mama huyo kwani lilikuwa kubwa sana
kiasi cha kuhisi kulikuwa na tatizo fulani. Ndipo walipoamua kuanza
kumfanyia uchunguzi. Baada ya kupima ujauzito huo kwa kutumia mashine ya ultra sound
(kamera ya mionzi), waliona ni kweli tumboni kuna watoto wenye maumbo
yasiyoeleweka hivyo walitaka kumsafirisha kumpeleka Hospitali ya Mkoa wa
Tanga, Bombo lakini walishindwa kutokana na hali yake. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz
Anasema baada ya kugundua kuwa hawataweza
kumsafirisha kutokana na hali yake, ilibidi wamuweke katika ulisimamizi
maalumu hadi siku ya kujifungua. Alijifungua kwa njia ya upasuaji. Katika upasuaji, madaktari walimtoa mtoto wa kwanza mwenye umbo la ajabu akiwa na kilo sita na wa pili akiwa na kilo 1.5. Anafafanua kuwa mtoto alipotolewa tumboni ingawa
hakuwa wa kawaida, alikuwa anapumua. Baada ya muda alianza kutoka maji
na saa moja baadaye alifariki dunia. Mtoto mwingine aliishi kwa siku
moja na akafariki.
“Alikuwa na kilo sita pia alikuwa amevimba sana.
Huu ni uzito mkubwa sana kwa mtoto. Baada ya muda mfupi alianza kutoka
maji hadi mwili ukapungua kiasi na baadaye alifariki. Mwenzie aliendelea
kuishi kwa saa 24,” anasema Dk Mushi. Mtoto huyo alizaliwa akiwa na miguu yote miwili,
lakini iliyoungana na kichwa chenye mdomo na masikio yanayoonekana kwa
mbali. Hana kiuno wala mikono.
Dk Mushi anasema kuwa zipo sababu nyingi za kitaalamu ambazo
zinaweza kusababisha hali hiyo kutokea na kusema kuwa miongoni mwa
sababu hizi ni umri mkubwa wa mwanamke. Anasema mama mwenye umri wa
miaka kuanzia 45-50 anashauriwa kupumzika kuzaa, kumeza dawa kali bila
ushauri wa daktari miezi mitatu baada ya mimba kutunga na sababu
nyingine ni mama mjamzito kuwa ameshajifungua watoto wengine wengi au
ameshabeba mimba zaidi ya saba.
Anasema mama huyo tayari alishabeba mimba zaidi ya
10 na baadhi ziliharibika. Hiyo ni dalili ya kutosha kuwa alipaswa
kuacha na ikiwezekana kufunga kabisa kizazi ili kuepukana na madhara
zaidi ya uzazi.
Dk Mushi anaeleza kuwa kitu kingine ni uelewa
mdogo wa jamii kuhusu masuala ya uzazi, kwani wapo baadhi ya wanandoa
hawafahamu umuhimu wa kupanga uzazi na badala yake wamekuwa wakipanga
uzazi kwa njia za kawaida bila ya ushauri wa daktari.
Kaimu mganga mkuu na mganga mfawidhi wa Hospitali
ya Wilaya ya Handeni, Dk Bakari Mdoe alisema kuwa katika miaka 20 ya
kazi ya udaktari, hiyo ni mara ya pili kukutana na kiumbe kama huyo,
lakini anasema huyo alizidi kwa kuwa maumbile yake hata hayawezi
kuelezeka. Dk Bakari anasema haieleweki mtoto huyo aliathirika na nini hadi akazaliwa akiwa na umbile hilo.
Mwajuma aelezea kisa kizima
Alipohojiwa kuhusu suala hilo, mwanamke huyo
alisema mara ya kwanza aliona kuwa amebeba mimba ya kawaida na hakukukwa
na tatizo lolote lakini muda ulipokuwa unasonga mbele alishangaa kuona
ujauzito ule unakuwa mzito sana. Anasema hali hiyo ilimtisha naye akaamua
kukimbilia hospitalini hapo kujua hatima yake, lakini hakupewa jibu la
uhakika badala yake aliambiwa abakie hospitalini.
Anasema kuwa mpaka siku ya kujifungua alijua ni
watoto wa kawaida na aliposhindwa kujifungua kwa njia ya kawaida na
kupelekwa chumba cha upasuaji, ndio akapewa taarifa kuwa kati ya watoto
wake wawili, mmoja si wa kawaida, jambo ambalo lilimpa mshituko kidogo
lakini ilibidi akubali baadaye kuwa hiyo ni kazi ya Mungu na hakuhusisha
na ushirikina.
Anasema hakuwahi kutumia dawa zozote kali na alikuwa anahudhuria kliniki kama kawaida na kufuata masharti yote ya ujauzito. Kwa sasa mama huyo amekubali ushauri wa kufunga
kizazi kabisa kwani historia ya uzazi wake inaonyesha hajapata mtoto
tangu ashike ujauzito wa 10.
Mama huyo, ambae pamoja na mumewe wanajishuhulisha
na kilimo, anasema alifanikwa kupata watoto nane, wakiwemo watano wa
kiume na watatu wa kike. Alibahatika kupata mapacha katika mimba yake ya
nne. “Nimeamua kukubali kufunga kizazi kwa kuwa nimechoka. Tangu
mimba ya 10 hadi hii ya juzi sifanikiwi kupata mtoto zaidi ya matatizo,
hivyo ngoja nipumzike hawa ambao Mungu amenijalia wanatosha sasa,”
alisema. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz
Aliyevunja Rekodi
Na Rajabu Athuman, Mwananchi
Hata hivyo, anaeleza kuwa katika kipindi chote cha
uzazi wake, hajawahi kukutana na elimu yoyote ya uzazi wa mpango na
kwamba endapo kama angeipata, labda asingepata matatizo hayo. Aidha anasema katika mimba zote 13 ni mbili tu
ndio alibahatika kujifungulia hospitalini, na zilizobaki 11
alijifungulia nyumbani kwa uangalizi wa wakunga wa jadi.
Daktari ashauri
Dk Mdoe anatoa ushauri kwa wakina mama na waume zao kujenga tabia ya kwenda kliniki kujifunza uzazi wa mpango. Anasema kuwa ni vema kujenga tabia hizo mapema
kwani zinaweza kuwasaidia kwa kufuatilia maendeleo ya mtoto tumboni,
kuliko kukaa nyumbani kwani mama mjamzito anaweza kupata matatizo
makubwa bila kama ambayo yamekuwa yakimtokea mwanamke huyu.
Aliyevunja Rekodi
Raia wa India, Rajo Devi ndiye mwanamke aliyevunja rekodi mwaka juzi ya kuzaa akiwa na umri mkubwa kuliko wengine duniani. Mwanamke huyo alishika ujauzito akiwa na umri wa
miaka 69. Ujauzito huo uliweka rehani uhai wake kwani isingekuwa
uangalizi mzuri wa madaktari, mwanamke huyo angepoteza maisha. Kama
ilivyo kwa wanawake wengi, mwanamke huyo alishika ujauzito baada ya
kufanyiwa upandikizaji wa mayai (IVF).
Pamoja na kuwa madaktari walitabiri mwanamke huyo
angekufa mapema kwasababu ya zoezi zima la kumpatia ujauzito kumgharimu
nguvu nyingi, mwanamke huyo yupo hai mpaka sasa na binti aliyemzaa,
Naveen ameanza shule. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz
No comments:
Post a Comment