Picha na Maktaba
Watu watano wasiofahamika wanaodhaniwa ni wezi, wamemvamia dereva wa lori la mafuta, Stephano John eneo la Kibamba, Barabara Kuu ya Dar es Salaam -Morogoro alipokuwa katika foleni na kisha kumpiga, kumjeruhi sehemu kadhaa za mwili, kumfunga kamba na kumtupa mtaroni.

Ilielezwa kuwa baada ya kumfunga kamba, wahalifu
hao walimdhibiti ndani ya lori na kutembea naye umbali wa kilomita moja
walipofika maeneo ya Kiluvya ambako walimtupa katika mtaro na kuendelea
na safari. Walifika mizani Kibaha wakapima uzito wa gari kama kawaida na
kutokomea.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Ulrich Matei
alisema tukio hilo lilitokea saa mbili usiku wakati dereva huyo akiwa
kwenye foleni na lori lake aina ya Scania lililokuwa na tela pia
lilikuwa na shehena ya petroli lita zaidi ya 39,000.
“Wakati dereva akiwa katika mwendo wa polepole
kwenye foleni ya malori kuingia mizani, alivamiwa ghafla na watu watano
waliofungua mlango na kuingia ndani.
“Wakati dereva akishangaa, walimnyanyua kwenye kiti na kumweka kiti cha nyuma na wakimtaka kukaa kimya,” alisema. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz