Kocha wa Yanga, Hans van Pluijm
Kocha wa Yanga, Hans van Pluijm na mwenzake Patrick Phiri wa Simba wametamba kuibuka na ushindi dhidi ya Azam na Kagera Sugar wakati mechi za Ligi Kuu ya Vodacom zitakapoingia raundi ya nane kuanzia kesho.

Pluijm alisema kuwa anaiheshimu Azam FC kama moja
ya timu bora kwenye ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, lakini hana hofu
yoyote.
“Nawaandaa vyema vijana wangu waibuke na ushindi
kwenye pambalo hilo kwa sababu litatuweka kwenye nafasi nzuri nje na
ndani ya uwanja,” alisema Pluij
m. Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz,
ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali
na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715
221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.
Pluijm aliongeza kuwa moja ya mkakati wake hivi
sasa ni kuhakikisha kuwa kila mchezaji wa kikosi hicho anakuwa fiti kwa
asilimia mia moja, ili kuwa na kikosi kikubwa kwa ajili ya mashindano ya
ndani pamoja na ya kimataifa.
“Nataka wote wawe fiti na pia kila mchezaji
nitampa nafasi ili niwe na wigo mpana wa uteuzi wa wachezaji wa kikosi
cha kwanza kuliko kuwa na kikosi kidogo ambacho kinaweza kukugharimu
pale timu inapopata majeruhi au mchezaji fulani anapokosekana.”
Naye Phiri alisema kwa kujiamini kuwa sasa matokeo
ya sare yatabaki historia katika kikosi chake kutokana na usajili mzuri
waliofanya.
Simba ambayo katika mechi saba za raundi ya kwanza
ilipata sare sita na kushinda moja, kesho itakuwa na kibarua kizito
mbele ya Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika
mwendelezo wa Ligi Kuu.
Kikosi chote cha Simba kilikuwa kambini Zanzibar
isipokuwa mshambuliaji Mganda, Emmanuel Okwi ambaye imeelezwa kuwa yupo
jijini Dar es Salaam akitokea Uganda ambako alikwenda kufunga ndoa.
Waganda wengine beki Juuko Murshid na winga Simon Sserunkuma walijiunga na kambi hiyo juzi na kuanza mazoezi na wenzao.
Phiri alisema anaamini timu yake itafanya vizuri na kusahau yaliyopita katika kuhakikisha wanamaliza katika nafasi tatu za juu. Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz,
ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali
na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715
221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.
No comments:
Post a Comment