Kocha Marcio Maximo amesema hana
kinyongo na uamuzi wa uongozi wa Yanga kumuondoa, ingawa umefuta ghafla
mkakati wa kutaka klabu hiyo iendeshwa kwa weledi.
Maximo na msaidizi wake Leonard Neiva
walisitishiwa mikataba yao baada ya Yanga kufungwa na Simba 2-0 katika
mchezo wa Nani Mtani Jembe mwezi huu, ikiwa ni takriban miezi mitano
tangu aje nchini.
Akizungumza muda mfupi kabla ya kupanda ndege
kurudi kwao Brazil jana, Maximo alisema hana kinyongo na uamuzi huo,
lakini akaitaka klabu hiyo kongwe kuendeleza soka la vijana na
kutengeneza mindombinu kama inataka kupata mafanikio makubwa katika
soka.
Alisema katika muda mfupi aliokuwa klabu hiyo,
alijenga misingi ya utendaji kazi wa kisasa ndani na nje ya uwanja kwa
wachezaji ili waweze kujitambua katika kazi yao, lakini jambo hilo
limeishia njiani. Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz,
ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali
na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715
221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.
“Katika miezi sita niliyokuwa na timu, nilijaribu
kujenga weledi ndani na nje ya uwanja, tulifanya kazi kubwa ya kujaribu
kutengeneza miundombinu, lakini tulishindwa kuwashawishi viongozi wote,”
alisema Maximo ambaye timu yake ililazimika kuhama viwanja kwa ajili ya
mazoezi kutokana na Uwanja wa Kaunda kuwa katika hali mbaya.
Yanga bado inapambana na mamlaka za jiji ikidai
iongezewe eneo ili ijenge uwanja wa kisasa, maombi ambayo yamekataliwa
na hivyo timu kulazimika kukodi viwanja tofauti kwa ajili ya mazoezi.
“Hii inatokana na ukweli kuwa baadhi ya viongozi
hawakupenda yale tuliyokuwa tunayafanya. Labda sisi hatukuwa makocha wa
aina yao ndio maana walichukua uamuzi waliouchukua. Hatuna kinyongo hata
kidogo. Tutakuwa sehemu ya timu hiyo na pale watakapotaka ushauri wetu
tutakuwa tayari kutoa,” alisema kocha huyo wa zamani wa timu ya taifa.
Alisema uamuzi uliochukuliwa ni kawaida kwa kuwa ni sehemu ya changamoto katika maisha ya ukocha pamoja.
“Ili kupata kazi ya ukocha, lazima kutakuwa na
tukio la kufukuza kocha. Kuondoka kwetu sisi kuna watu wengine
wameingia. Maisha bado yanaendelea. Si ajabu kwani kuna ushahidi kuwa
baadhi ya makocha walikatishiwa mikataba yao na kurejea tena katika timu
hiyo hiyo, kama ilivyotokea kwa Jose Mourinho, aliondoka Chelsea na
kurejea tena kutokana na uongozi kutambua kile alichokuwa anakifanya
kabla hajasitishiwa mkataba wake,” alisema.
Maximo anaondoka akiwa ameiacha Yanga katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu. Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz,
ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali
na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715
221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.
Na Mwananchi
Na Mwananchi
No comments:
Post a Comment