Kesi ya kuchoma moto bendera ya CCM
inayomkabili Mbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nassari jana
iliahirishwa na Ofisa Mtendaji wa Kata ya Maji ya Chai, Ndikilo Mbise
kutokana na Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo ya Maji ya Chai, David Mwita
kuwa safarini.
Akiahirisha kesi hiyo, Mbise alisema itatajwa tena
Januari 20 mwakani.Mbise alisema Hakimu Mwita amepata msiba, hivyo
amekwenda nyumbani kwao mkoani Mara huku, hakimu mwingine wa mahakama
hiyo akiwa likizo.
Mbise alisema ameahirisha kesi na kuipangia tarehe nyingine kwa kuwa ni mlinzi wa amani wa eneo hio.
Katika kesi hiyo, Nassari ambaye hakuhudhuria
mahakamani hapo kutokana na kuwa safarini, anatuhumiwa kuchoma bendera
ya CCM Desemba 15, saa 11 jioni katika eneo la Maji ya Chai. Bendera
hiyo yenye thamani ya Sh250,000 ilikuwa mali ya Raphael Moses.
Ilielezwa mahakamani hapo kuwa mtuhumiwa ataendelea kuwa nje kwa dhamana ya wadhamini watatu ya Sh1.5 milioni kila mmoja. Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz,
ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali
na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715
221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.
No comments:
Post a Comment