Kocha Mkuu wa Mbeya City, Juma Mwambusi amesema tatizo kubwa kwa sasa katika kikosi chake ni safu ya ushambuliaji ambayo ameendelea kuisuka ili wafanye vyema Ligi Kuu Bara itakapoendelea.
Akizungumza na gazeti hili jana, Mwambusi alisema
vijana wake wapo ‘fiti’ na wana ari mpya ya kurudisha heshima yao kwa
mashabiki wao huku akisema kuteleza siyo kuanguka, kwani yalitokea hivi
karibuni ndani ya klabu hiyo yamepita na sasa wanakuja kivingine.
“Ukiangalia mechi zilizopita tulipata mabao mawili
tu, na raha ya mpira wa sasa ni kufunga mabao mengi, hivyo nimeona
ushambuliaji ni tatizo kubwa, lakini tunaendelea na maboresho katika
safu hii,” alisema Mwambusi. Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz,
ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali
na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715
221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.
Mwambusi pia alipinga vikali hoja inayotolewa na mashabiki na wadau mbalimbali kwamba Mbeya City ni timu kubwa katika Ligi Kuu.
“Mbeya City bado ni timu changa kwenye ligi, hivyo
hata wale wanaoihukumu kwa kufanya vibaya wanakosea ila wanapaswa kuwa
na subira kwanza, ndiyo kwanza tuna mwaka mmoja tu kwenye ligi hii hivyo
bado ni changa sana, wakubwa na wakongwe ni kama vile Mtibwa Sugar,
ambayo ina zaidi ya miaka 10 katika ligi, na sisi laiti tungekuwa na
miaka walau minne katika ligi tulipaswa kuhukumiwa, lakini siyo kama
ambavyo wanatuhukumu.”
Kuhusu usajili alioufanya katika dirisha dogo
Mwambusi alisema haumaanishi kwamba kikosi cha awali kilikuwa kibaya ila
ni maboresho madogo dogo na kuimarisha zaidi kikosi chake. Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz,
ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali
na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715
221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.
Na Mwananchi
Na Mwananchi
No comments:
Post a Comment