Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo
WAZIRI wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, amesema vijiji
45 mkoani Mara vinatarajiwa kuunganishiwa na huduma ya umeme kupitia
Wakala wa Nishati Vijijini (REA).
Alisema hayo katika ziara yake ya siku sita katika mkoa wa Mara,
lengo likiwa ni kukagua na kuzindua miradi ya umeme vijijini
inayosimamiwa na REA awamu ya pili kwa kushirikiana na Shirika la Umeme
Nchini (Tanesco).
Alisema ziara yake iliyohusisha wilaya za Musoma, Tarime, Rorya,
Bunda na Serengeti, ililenga kubaini na kukagua mahitaji ya umeme katika
wilaya hizo ili vijiji vilivyokosa umeme kwenye awamu ya pili,
viingizwe katika awamu nyingine ya umeme vijijini.
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz,
ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali
na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715
221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.
Alieleza kuwa Wizara imekuwa ikisambaza umeme katika kila Mkoa na
Wilaya za Tanzania kwa awamu, kulingana na mahitaji na idadi ya watu
katika maeneo hayo.
Alisema kwa sasa umeme unaosambazwa upo katika awamu ya pili, ambapo awamu ya tatu itakuja baada awamu ya pili kumalizika.
Alisema vipaumbele vinavyotolewa katika uunganishaji wa umeme
vijijini ni maeneo yenye huduma muhimu za kijamii kama shule, vituo vya
afya, makanisa, misikiti, ofisi za vijiji na kata na sehemu zenye miradi
ya maji.
“Lengo letu kuu kwanza ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma za
jamii kwa urahisi na baada ya kuboreshwa kwa huduma hizo tunakwenda
kuwaunganishia umeme wananchi mmoja mmoja, ikiwa ni mkakati wa
kuhakikisha maisha ya wananchi yanaboreshwa kupitia nishati ya umeme,”
alisema Muhongo
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz,
ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali
na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715
221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.
No comments:
Post a Comment