Monday, June 20, 2016
YANGA YASHINDWA KUTAMBA KWA WAARABU YAPIGWA 1-0
Mabingwa wa soka la Tanzania bara Yanga SC wameanza vibaya kampeni
zao za kuwania kombe la Shirikisho Afrika baada ya kupoteza mchezo wao
wa kwanza kwa bao 1-0 dhidi ya MO Bejaia ukiwa ni chezo wa Kundi A.
Matokeo hayo yanaiacha Yanga katika nafasi ya tatu huku TP Mazembe
wakiwa ndiyo vinara wa Kundi baada ya kushinda mchezo wao kwa magoli 3-0
dhidi ya Medeama ambayo inaburuza mkia.
Mchezo ujao wa Yanga utakuwa nyumbani (Dar es Salaam) June 28 itakapowaalika TP Mazembe kwenye uwanja wa taifa.
Saturday, May 14, 2016
HII NDIO YANGAAA.... WAKABIDHIWA RASMI KOMBE LA UBINGWA WA VPL
Waziri wa Kilimo na Mifugo Mh.
Mwigulu Nchemba (kushoto) ambaye alikuwa mgeni rasmi wa mchezo huo akikabidhi
kombe hilo kwa nahodha Nadir Haroub ‘Cannavaro’ baada ya kumalizika kwa mchezo
kati ya Ndanda FC Yanga dhidi ya Yanga uliomalizika kwa timu hizo kutoka sare
ya kufungana magoli 2-2.
Kikosi cha Yanga wakishangilia
baada ya kukabidhiwa kombe lao.
Donald Ngoma (kushoto) na Simon Msuva wakipongezana wakati wa
mchezo wa leo.
Yanga imekabidhiwa taji lao la ubingwa wa VPL msimu wa 2015-16 baada ya kufanikiwa kulitetea taji hilo ambalo walilitwaa msimu uliopita. Yanga imepewa kombe hilo ikiwa na pointi 74 huku ikiwa na mchezo mmoja mkononi baada ya kuifunga Ndanda FC kwenye uwanja wa taifa.
Ndanda walianza kupata goli kwa mkwaju wa penati Omary Mponda lakini bao hilo lilisawazishwa na Simon Msuva dakika chache baadaye. Donald Ngoma akaifungia Yanga bao la pili na kuiweka mbele klabu yake lakini Salum Minely akachomoa bao hilo na kuilazimisha Yanga kwenda sare kwenye uwanja wa taifa ambao Ndanda ndiyo walikuwa wenyeji katika mchezo huo.
Waziri wa Kilimo na Mifugo Mh. Mwigulu Nchemba ambaye alikuwa mgeni rasmi wa mchezo huo alilikabidhi kombe hilo kwa nahodha Nadir Haroub ‘Cannavaro’ baada ya kumalizika kwa mchezo kati ya Ndanda FC Yanga dhidi ya Yanga uliomalizika kwa timu hizo kutoka sare ya kufungana magoli 2-2.
Ubingwa huo unawafanya Azam FC kulikosa taji hilo ndani ya misimu miwili mfululizon wakati Simba wao wameendelea kulikosa taji hilo ndani ya misimu minne mfululizo.
Yanga imekabidhiwa taji lao la ubingwa wa VPL msimu wa 2015-16 baada ya kufanikiwa kulitetea taji hilo ambalo walilitwaa msimu uliopita. Yanga imepewa kombe hilo ikiwa na pointi 74 huku ikiwa na mchezo mmoja mkononi baada ya kuifunga Ndanda FC kwenye uwanja wa taifa.
Ndanda walianza kupata goli kwa mkwaju wa penati Omary Mponda lakini bao hilo lilisawazishwa na Simon Msuva dakika chache baadaye. Donald Ngoma akaifungia Yanga bao la pili na kuiweka mbele klabu yake lakini Salum Minely akachomoa bao hilo na kuilazimisha Yanga kwenda sare kwenye uwanja wa taifa ambao Ndanda ndiyo walikuwa wenyeji katika mchezo huo.
Waziri wa Kilimo na Mifugo Mh. Mwigulu Nchemba ambaye alikuwa mgeni rasmi wa mchezo huo alilikabidhi kombe hilo kwa nahodha Nadir Haroub ‘Cannavaro’ baada ya kumalizika kwa mchezo kati ya Ndanda FC Yanga dhidi ya Yanga uliomalizika kwa timu hizo kutoka sare ya kufungana magoli 2-2.
Ubingwa huo unawafanya Azam FC kulikosa taji hilo ndani ya misimu miwili mfululizon wakati Simba wao wameendelea kulikosa taji hilo ndani ya misimu minne mfululizo.
KAGAME AKANA KUWASAIDIA WAASI WA BURUNDI
Rais
wa Rwanda Paul Kagame
Rais wa Rwanda
Paul Kagame amekana madai yaliotolewa na Umoja wa Mataifa kwamba taifa lake
linaendelea kuwasaidia waasi katika nchi jirani ya Burundi.
Kagame amesema kuwa tatizo la Burundi
linatoka ndani ya nchi hiyo, na sio nje. Burundi imekabiliwa na mgogoro mbaya
wa kisiasa tangu rais Pierre Nkurunziza kuamua kupigania muhula mwengine mwaka
uliopita.
Ni mwaka mmoja kamili tangu rais Nkurunziza
kuepekua jaribio la mapinduzi. Rwanda ilikana madai kama hayo kuhusu kuwaunga
mkono waasi katika ripoti ya awali ya Umoja wa Mataifa mnamo mwezi Februari.
Pia Kagame amekosoa wachapishaji wa ripoti
hiyo ambayo inatarajiwa kuwasilishwa katika baraza la usalama la Umoja wa
Mataifa baadaye,ikisema mda wake ungetumika vyema kuangazia matatizo
yanayokumba mataifa badala ya kuyazidisha.
Ripoti hiyo iliopatikana na chombo cha habari
cha Reuters imeishtumu Rwanda kwa kutoa mafunzo pamoja na usaidizi wa kifedha
kipindi chote cha mwaka 2016 kwa waasi wanaolenga kumuondoa madarakani rais
Pierre Nkurunziza.
UN "UHUSIANO WA IS NA BOKO HARAM NI TISHIO"
Baraza la
usalama la Umoja wa Mataifa limeelezea wasiwasi wake kuhusu kasi ya kuimarika
kwa ushirikiano kati ya kundi la wapiganaji la Boko Haram nchini Nigeria na
lile la Islamic State, wakati Nigeria inaandaa kongamano la kupambana na kundi
hilo la kigaidi.
Katika taarifa kwa vyombo vya habari, baraza
hilo la wanachama 15 limesema kuwa Boko Haram linaendelea kuwa tishio kwa amani
na usalama wa mataifa ya Afrika Magharibi na Afrika ya kati.
Boko Haram lilitangaza utiifu wake kwa
Islamic State mwaka jana, na inaripoitiwa kuwa liliwatuma wapiganaji wake
kuungana na Islamic State nchini Libya.
Baraza hilo pia limekaribisha kongamano
lililoandaliwa na rais wa Nigeria Mohamadu Buhari siku ya Jumamosi, kuangazia
upya jitihada za kupambana na wapiganaji hao. Kongamano hilo litahudhuriwa na
viongozi wa kikanda pamoja na rais wa ufaransa Francois Hollande.
Thursday, May 05, 2016
SNURA AWAOMBA RADHI WATANZANIA, AWASILISHA VIDEO SAFI YA CHURA BASATA
Snura amewaomba radhi watanzania kwa video ya wimbo wake ‘Chura’ inayowadhalilisha wanawake na iliyo kinyume na maadili. Muimbaji huyo amekutana na waandishi wa habari Alhamis hii kwenye ukumbi wa Habari Maelezo jijini Dar es Salaam.
Jana
video na wimbo huo vilifungiwa na wizara ya habari, utamaduni, sanaa na
michezo kwa madai kuwa inakiuka maadili ya Kitanzania. Pia alizuiwa
kufanya maenesho ya hadhara kwakuwa hajajisajili kwenye baraza la sanaa
la taifa, BASATA.
Kwenye
mkutano huo na waandishi wa habari, Snura amedai kuwa tayari
amekamilisha mchakato wa usajili na BASATA imempa kibali. Pia amedai
kuwa amewasilisha video mpya ya wimbo huo kwa bodi ya filamu ya Tanzania
ambayo itaikagua. Tangaza
biashara yako hapa. Pia like page yetu ya facebook Jambo Tz. tu-follow
instagram @jambotz.
HUKUMU KESI YA KAFULILA MEI 17
Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Tabora inayosikiliza kesi ya
kupinga matokeo ya uchaguzi wa Jimbo la Kigoma Kusini iliyofunguliwa na
aliyekuwa mgombea kupitia Chama cha NCCR-Mageuzi, David Kafulila
inatarajia kutoa hukumu Mei 17, mwaka huu.
Jaji wa mahakama hiyo anayesikiliza kesi hiyo mjini Kigoma, Ferdinand
Wambali, alisema kuwa amepanga kutoa hukumu tarehe hiyo baada ya pande
zote mbili kuwasilisha ushahidi na maelezo yao.
Baada ya kukamilika kwa ushahidi huo, Jaji Wambari aliomba kupatiwa
muda wa kutosha kupitia ushahidi na vielelezo vilivyowasilishwa
mahakamani hapo ili aweze kutoa hukumu ya haki.
Aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Uvinza, Ruben Mfune ambaye
alikuwa msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo ni mshtakiwa wa tatu katika
kesi hiyo. Katika kesi hiyo namba 2 ya mwaka 2015, Kafulila anaishawishi
mahakama itengue matokeo yaliyompa ushindi aliyekuwa mgombea wa CCM,
Hasna Mwilima badala yake imtangaze yeye kama mshindi halali wa jimbo
hilo.
Walalamikiwa katika kesi hiyo ni pamoja na Mbunge wa jimbo hilo
Hasna, aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Uvinza, Ruben Mfune ambaye
alikuwa msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo na Mwanasheria wa Serikali
ambaye anaiwakilisha Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Katika kesi hiyo, Wakili Kenedy Fungamtama anamtetea Husna huku
Kafulila akitetewa na mawakili watatu, Profesa Abdallah Safari, Tundu
Lissu na Daniel Rumenyela.
VYUO VIKUU BORA DUNIA
Orodha
mpya ya vyuo vikuu bora zaidi
duniani ya Times Higher Education, kwa kuangazia sifa za chuo kikuu
husika, imetolewa, huku vyuo vikuu kutoka bara Asia vikiimarika sana.
Mwaka huu, kuna vyuo vikuu 17 kutoka Asia vilivyomo kwenye orodha ya
vyuo 100 bora, likiwa ongezeko kutoka vyuo 10 mwaka jana.
Kwa
mara ya kwanza, kuna chuo kikuu kutoka Uchina katika 20 bora, Chuo
Kikuu cha Tsinghua University kutoka Beijing ambacho kimo nambari 18.
Vyuo vikuu vya Marekani bado vinatawala orodha hiyo, chuo kikuu cha
Harvard kikiwa ndicho kinachoongoza. Vifuatavyo ni vyuo vikuu bora 100.
1 . Harvard University
Marekani2 . Massachusetts Institute of Technology
Marekani3. Stanford University
Marekani4. University of Cambridge
UingerezaWAPENZI WA JINSIA MOJA WAPINGA UKAGUZI WA 'TUPU ZA NYUMA'
Wanaume wawili
wanaosema kuwa maafisa wa polisi wa Kenya waliwalazimisha kufanyiwa
ukaguzi wa tupu ya nyuma ili kubaini kwamba walishiriki katika ngono ya
mapenzi ya jinsia moja wameanzisha kesi mahakamani wakitaka ukaguzi huo
kuwa ukiukaji wa katiba.
Wanasema kuwa walilazimishwa kufanyiwa
ukaguzi wa magonjwa ya virusi vya ukimwi na Hepatitis kufuatia kukamatwa
kwao mnamo mwezi Februari 2015 baada ya kushukiwa kwamba wanashiriki
katika ngono ya mapenzi ya jinsia moja.
Vitendo
vya wapenzi wa jinsia moja kushiriki ngono ni kinyume na sheria nchini
Kenya na adhabu ya makosa hayo ni miaka 14 jela. Mahakama ya Mombasa
imewapatia mawakili wa serikali wiki moja kutoa jibu. Chini
ya sheria ya kimataifa, ukaguzi wa lazima katika tupu ya nyuma ni
kitendo cha kikatili,unyama na ni sawa na mateso kulingana na kundi la
haki za kibinaadamu Human Wrights Watch
KATUMBI ATANGAZA KUWANIA URAIS CONGO
Mwanasiasa mashuhuri nchini Jamhuri
ya Demokrasi ya Congo Moise Katumbi amethibitisha kuwa atagombea urais
kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Novemba.
Mfanyabiashara
huyo na gavana wa zamani wa jimbo la Katanga alitoa
tangazo hilo kupitia kwa mitandao ya kijamii. Muungano wa vyama kadha
vya upinzani uliamua kumuidhinisha Bw Katumbi kuwa mgombea mwezi Machi.
Bw Katumbi, akitangaza kuwania kwake, amepuuzilia mbali madai kwamba
alipokuwa waziri wa hati alitumia mamluki kutoka nje akisema habari hizo
ni za uongo. Kwa mujibu wa
katiba ya nchi hiyo Rais Joseph Kabila anatakiwa kuondoka madarakani
mwaka huu lakini wapinzani wake wana hofu kuwa huenda ana mipango ya
kusalia madarakani.
CHURA AMPONZA 'SNURA MAJANGA' AFUNGIWA KUFANYA KAZI ZA SANAA
Serikali imesitisha wimbo na video ya ‘Chura’ wa msanii,
Snura Mushi ‘Snura Majanga’, kuchezwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari hadi
itakapofanyiwa marekebisho. Wimbo na video hiyo umetokana na maudhui ya
utengenezwaji wake ambayo hayaendani na maadili ya Mtanzania. Tangaza biashara
yako hapa. Pia like page yetu ya facebook Jambo Tz. tu-follow
instagram @jambotz.
Pia Serikali imesitisha maonyesho yote ya
hadhara ya msanii huyo, mpaka atakapokamilisha taratibu za usajili wa kazi zake
za sanaa katika Baraza la Sanaa la Taifa (Basata). Licha ya hivyo, Serikali
imewataka wasanii wajiulize kabla ya kubuni kazi zao za sanaa kwa kufikiria
wazazi, ndugu, jamaa na marafiki zao namna watakavyozipokea.
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano
serikalini, Zawadi Msalla, aliwaambia waandishi wa habari kwamba wasanii
wanapotunga nyimbo zao wavae nafasi za wanaowadhalilisha na waelewe kwamba
sanaa si uwanja wa kudhalilisha watu. Tangaza biashara yako hapa. Pia like page yetu ya facebook Jambo Tz. tu-follow
instagram @jambotz.
MAN CITY WACHAPWA 1-0 NA REAL MADRID
Manchester City wameshindwa kufika
katika fainali za kwanza za klabu bingwa barani Ulaya (UEFA) baada ya
kutolewa na mabingwa mara 10 wa michuano hiyo Real Madrid katika mchezo
uliokua wa kuvutia tena wa aina yake. Walichapwa 1-0.
Baada ya
kutokuwa na ushindi wowote katika mzunguko wa kwanza, Real Madrid
walianza kuongoza kipindi cha kwanza kufuatia mpira wa krosi uliopigwa
na Gareth Bale kumbabatiza kiungo wa City Fernando na kuingia nyavuni.
Real waliutawala mchezo huku mpira wa kichwa uliopigwa na Bale ukigonga
mwamba na baadaye mlinda mlango wa City Joe Hart akiondoa mikwaju ya
Luka Modric na Cristiano Ronaldo.
Klabu hiyo ya Uingereza ilikuwa ikihitaji bao moja muhimu la ugenini
hususan katika dakika za lala salama kuelekea fainali,lakini hilo
halikuweza kufanikiwa licha ya kushangiliwa na mashabiki wake wapatao
4,500.
Madrid walipata wakati mgumu kidogo pale mkwaju mkali wa
Sergio Aguero ulipogonga nyavu za juu za lango la Madrid. Real sasa
watakutana na Atletico katika uwanja wa San Siro tar 28 Mei, hii ikiwa
ni kama marudio ya fainali za mwaka 2014 ambapo Real walishinda kwa
mabao 4-1 baada ya muda wa nyongeza.
Tuesday, May 03, 2016
WAZIRI MAHIGA AMTETEA MKEWE
WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Dk. Augustine Mahiga, amezungumzia sakata la
mke wake kudaiwa kumtukana askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani.
Akizungumza na mwwandishi wa habari hii jana mjini hapa, Dk. Mahiga alisema kwamba mke wake alipishana kauli na askari huyo aliyefahamika kwa jina la Deogratius Mbango, na hakutoa lugha ya matusi kama inavyodaiwa.
Alisema baada ya kupokea taarifa hiyo, alifuatilia ili kujua ukweli, ikiwamo kusikiliza sauti ya majibizano baina ya askari huyo na mkewe, ambapo alibaini kuwa walipishana kauli. Tangaza biashara yako hapa. Pia like page yetu ya facebook Jambo Tz. tu-follow instagram @jambotz.
Akizungumza na mwwandishi wa habari hii jana mjini hapa, Dk. Mahiga alisema kwamba mke wake alipishana kauli na askari huyo aliyefahamika kwa jina la Deogratius Mbango, na hakutoa lugha ya matusi kama inavyodaiwa.
Alisema baada ya kupokea taarifa hiyo, alifuatilia ili kujua ukweli, ikiwamo kusikiliza sauti ya majibizano baina ya askari huyo na mkewe, ambapo alibaini kuwa walipishana kauli. Tangaza biashara yako hapa. Pia like page yetu ya facebook Jambo Tz. tu-follow instagram @jambotz.
Subscribe to:
Posts (Atom)