Ligi
kuu ya Tanzania bara, maarufu kama Ligi Kuu ya Vodacom inaanza rasmi
mzunguko wa pili leo, Ijumaa baada ya kusitishwa tangu Novemba 7, 2014.
Hadi
ligi hiyo ilipositisha mzunguko wa kwanza, tayari timu 14 zinazoshiriki
ligi hiyo zilikuwa zimecheza michezo saba kila moja.Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Shirikisho la Kandanda nchini Tanzania, TFF, Simba ambayo ni miongoni mwa timu kongwe za ligi hiyo na ambayo katika mzunguko wa kwanza haikuwa na matokeo mazuri baada ya kwenda sare mara sita na kushinda mchezo mmoja na kujikusanyia pointi tisa ikishika nafasi ya saba katika msimamo wa ligi hiyo, leo inaikaribisha Kagera Sugar inayoshikilia nafasi ya tano katika pambano litakalofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Michezo mingine itafanyika katika viwanja mbalimbali kuanzia Ijumaa, Jumamosi na Jumapili wiki hii.
Mpaka sasa Mtibwa Sugar ndiyo inayoongoza ligi hiyo ya Vodacom baada ya kujikusanyia pointi 15, ikifuatiwa na Young Africans(Yanga) kwa kuwa na pointi 13 sawa na Azam mabingwa watetezi. Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.