Kikosi cha timu ya Azam ya Ligi Kuu ya Vodacom, Tanzania
Ligi
kuu ya Tanzania bara, maarufu kama Ligi Kuu ya Vodacom inaanza rasmi
mzunguko wa pili leo, Ijumaa baada ya kusitishwa tangu Novemba 7, 2014.
Hadi
ligi hiyo ilipositisha mzunguko wa kwanza, tayari timu 14 zinazoshiriki
ligi hiyo zilikuwa zimecheza michezo saba kila moja.Michezo mingine itafanyika katika viwanja mbalimbali kuanzia Ijumaa, Jumamosi na Jumapili wiki hii.
Mbeya City iliyotikisa msimu uliopita na kupata mashabiki wengi nchini Tanzania, imejikuta ikizibeba timu zote baada ya michezo saba ikiwa na pointi tano tu ikitanguliwa na timu za Ndanda na Tanzania Prisons zenye pointi sita kila moja.
Nao wapinzani wao wa jadi Yanga, imemtimua aliyekuwa kocha wake kutoka Brazil Marcio Maximo baada ya kufungwa mabao 2-0 na Simba katika mchezo wa Nani Mtani Jembe. Pia Yanga imesajili wachezaji mahiri akiwemo Amisi Tambwe ambaye katika mzunguko wa kwanza alichezea timu ya Simba lakini akaenguliwa katika usajili wa dirisha dogo.
Kinachosubiriwa na wapenzi na mashabiki wa timu hizo ni kwa kila timu kupata ushindi, kufikia ubingwa. Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.
No comments:
Post a Comment