Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri
Tanzania (KKKT), Dk Alex Malasusa amesema watanzania wengi hivi sasa
wamekosa kitu muhimu na cha thamani katika maisha yao, ambacho ni
kutokuwa na hofu ya Mungu.
Amesema kufuatia hali hiyo Tanzania imejikuta
ikiingia kwenye vitendo vya rushwa na ufisadi, huku viongozi waliopewa
dhamana na wananchi wakiweka mbele maslahi yao binafsi badala ya Taifa.
Askofu Malasusa ameyasema haya leo katika Kanisa
la Azania Front jijini Dar es Salaam wakati akitoa salamu na akihubiri
katika ibada ya Krisimasi ya kuadhimisha kuzaliwa kwa Yesu Kristo.
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

Malasusa amesema jamii ya watanzania kwa sasa ni
kama vile watu wamepofushwa macho maana wanachokifanya ni kama hawaoni,
kwani kila kiongozi amewekeza zaidi katika kujinufaisha yeye binafsi
badala ya kufanya kazi kwa uadilifu kwa lengo la kuleta ustawi kwa Taifa
na wananchi wake.
“Hofu ya Mungu ikitawala katika maisha yetu,
viongozi watatenda mambo mema, hofu ya Mungu ikitawala ndani ya mioyo
yetu hakika vitendo vya rushwa na ufisadi havitapata nafasi katika
nchini yetu nzuri Tanzania,”anasema Askofu Dk Malasusa.
Askofu Dk Malasusa anasema hakuna faida ya watu
kujilimbikizia fedha nyingi huku maelfu ya watanzania wakiendelea
kuteseka na kupata tabu kila kukicha, hivyo aliwasahi watanzania na
viongozi wote serikali kubadili fikra zao na kumuogopa Mungu ili
Tanzania ipone.
“Wakristo tunahitaji kusimama kwa ujasiri na
kukemea mabaya yote katika jamii yetu hata kama yanafanywa na marafiki
zetu kwa kuwa neno linatuagiza kufanya hivyo. Bwana anasema ‘woga ni
dhambi’, hivyo tuwe makini ili kuepuka dhambi hii yenye madhara kwa watu
wengi katika taifa hili,” alisisitiza Dk Malasusa.
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.
Na Mwananchi

No comments:
Post a Comment