Kamanda wa kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamedi Mpinga (kulia) akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam.
JESHI la Polisi kwa kushirikiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa
Nchi Kavu na Majini (SUMATRA), limewaadhibu wamiliki wa magari zaidi ya
21.
Mawakala wao wa kukata tiketi, wamesombwa na kuburuzwa mahakamani,
ambao baada ya kesi zao kusogeswa mbele, sasa wanasota mahabusu,
watakakokuwa hadi baada ya shamrashamra za kuukaribisha Mwaka mpya 2015.
Wakati mabasi mengi yakinaswa Morogoro, mawakala wa tiketi ambao pia
ni maarufu kama wapigadebe, wamekamatwa katika kikuo kikuu cha mabasi
yaendayo mikoani cha Ubungo, Dar es Salaam.
Hayo yamethibitishwa na Ofisa Mfawidhi wa Sumatra Mkoawa Morogoro,
Allen Mwanri aliyesema mabasi zaidi ya 21 yalikamatwa kwa makosa ya
mbalimbali, likiwemo kubwa la kuzidisha nauli na kutoza nauli kubwa.
Hata hivyo, alisema kila mmiliki wa basi lililokamatwa kwa kuzidisha
nauli na nauli kubwa, alitozwa adhabu ya kiasi cha Sh 250,000. Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz,
ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali
na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715
221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.
Alitaja wamiliki waliowajibishwa kwa kuzidisha nauli na namba za
mabasi kwenye mabano ni Kheri Kidinilo (T 292 AZY), Ngailo Express (T
366 BQD), Idd A. Fundi (T 853 DBY), Mohammed Trans kwa mabasi yake
mawili (T 738 AAP na T 647 AWD). Wengine na mabasi yao ni Omari Kilala
Ally (T277 AJR), Ayoub Ntomola (T590 BHJ), Patrick K.Kimei (T 615 BRK)
na Boadway Business Solution (T278 CLY).
Mabasi yaliyozidisha nauli kubwa ni Wegesa Iroga (T889 CNN) na
Stanley Membo (T233 CVH). Kwa mujibu wa Mwanri, wengine ni Seif Omary (
T211 AJT), NBS CO LTD (T183 BVZ), Nyehunge mwenye mabasi mawili (T 508
CSX na T400 AEL), BM Coach (T542 CUW), Joseph Makanga (T166 BNC), Hassan
Msofe (T819 CHY), Islam (T576 CVD), Abdallah Ally (T725 CXY) na Vicent
Lusinde (T874 DAM).
Hata hivyo, wakizungumza kwa nyakati tofauti, Kamanda wa Polisi wa
Mkoa wa Morogoro, Leonard Paul na Ofisa Mfawidhi wa Sumatra mkoa wa
Morogoro, walisema ukaguzi huo umelenga kukomesha baadhi ya wamiliki wa
mabasi ambao wanatumia kipindi cha sikukuu za mwisho wa mwaka, kukiuka
masharti ya leseni za usafirishaji wa abiria.
Wengi wasombwa Ubungo Kikosi cha Polisi cha Usalama Barabarani
kimeendelea kuwakamata watu waliokutwa wanauza tiketi kwa bei kubwa
katika Kituo Kikuu cha Mabasi yaendayo Mikoani cha Ubungo, ambapo hadi
jana watu 10 walikuwa wamekamatwa.
Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohammed Mpinga alisema
watu hao walipelekwa mahakamani na sasa wapo gereza la Segerea hadi
Januari 5 mwaka kesho, kesi zao zitakapotajwa tena.
Alitaja waliokamatwa kuwa ni Victor Kombe ambaye ni wakala wa KVC,
Mussa Msangi ambae ni karani wa tiketi za Happy Nation, Walter Nkya ni
karani wa tiketi za Ibra Line na Fredrick Lema ambae ni Karani wa Mbazi
Travel Coach.
Wengine ni Ramadhani Mbaga, Stephen Amos, Jane Gabriel, Kassim Azaria
ambao walikuwa na usafiri wa Toyota Noah, Kelvin Charles ni wakala
Islam, Mbaraka Tariba Kombo ambae nae ni wakala wa Islam. Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz,
ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali
na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715
221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.
Na Habari Leo
No comments:
Post a Comment