Wenyeviti watatu wa Kamati za
Bunge waliopendekezwa kuwajibishwa na Bunge hilo katika sakata la
Akaunti ya Tegeta Escrow wataondolewa katika nyadhifa zao ndani ya siku
21 zijazo, imeelezwa.
Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai alisema jana kuwa
utekelezaji wa maazimio ya Bunge kwa upande wa mhimili huo wa dola
utafanyiwa kazi mapema mwakani.
“Hilo litatekelezwa wakati wa Kamati za Bunge
ambazo zitaanza mwishoni mwa wiki ya pili ya Januari mwakani kwa kamati
husika kuchagua wenyeviti wapya.”
Wenyeviti hao ni wa Kamati ya Nishati na Madini,
Victor Mwambalaswa, William Ngeleja wa Katiba, Sheria na Utawala na
Andrew Chenge wa Kamati ya Bajeti. Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz,
ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali
na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715
221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.