Aliyekuwa
rais wa Marekani George H.W Bush amekimbizwa katika hospitali moja ya
Houston nchini Marekani baada ya kupatikana na tatizo la kupumua.
Kulingana na madaktari,Bush mwenye umri wa miaka 90 anachunguzwa katika hospitali ya Methodist.Alipelekwa katika hospitali hiyo na ambalensi jumanne usiku.
Wawakilishi wa Bush wanasema kuwa hatua hiyo ya kupelekwa hospitali ni kama tahadhari.
Rais huyo wa 41 ndio mzee kuwahi kuiongoza Marekani akimshinda Jimmy Carter kwa miezi michache.
Alihudumu kwa muhula mmoja baada ya kushindwa na Rais Bill Clinton.
Bush ambaye hawezi kutumia miguu yake,hivi majuzi alionekana amekaa katika kiti cha magurudumo katika hafla iliofanyika mwezi November katika chuo kikuu cha Texas na mwanawe aliyekuwa rais George W Bush. Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.
No comments:
Post a Comment