RAIS Jakaya Kikwete
RAIS Jakaya Kikwete amesema ni lazima watumishi wa umma wanaokiuka
maadili ya utumishi wa umma wawajibishwe ili iwe fundisho kwao na kwa
wengine.
Rais Kikwete aliyasema hayo Dar es Salaam juzi baada ya Mkuu wa Mkoa
wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki kumkaribisha kuzungumza na wazee wa
jiji hilo.
Awali kabla ya Rais kuzungumza, Sadiki katika hotuba yake alimwelezea
Rais jinsi Uchaguzi Mkuu wa Serikali za Mitaa ulivyofanyika jijini
mwake na kusema CCM imefanya vizuri kwa kuibuka na ushindi wa jumla ya
asilimia 75.
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz,
ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali
na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715
221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.
“Mheshimiwa Rais, katika ya mitaa 557 ya jiji hili, 555 ndiyo
iliyofanya uchaguzi hiyo miwili haikufanya kwa sababu mbalimbali na
matokeo ni kwamba CCM imeendelea kufanya vizuri tumepata ushindi wa
jumla ya asilimia 75,” alisema Sadiki.
Na kuongeza Chadema ilipata asilimia 14, CUF wao walipata asilimia 11
na NCCR-Mageuzi wao walipata asilimia 0.1. Akizungumzia suala zima la
uchaguzi huo nchini, Rais alivipongeza vyama vyote kwa ushiriki wao na
wale walioshinda aliwashauri kutafuta mbinu za kuwakomboa wananchi
waliowaamini na kuwapa kura.
Aidha, alipongeza uamuzi wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,
Tamisemi, Hawa Ghasia kwa kuchukua hatua dhidi ya watendaji wa umma
waliosababisha kuwapo kwa kasoro kwenye baadhi ya maeneo katika uchaguzi
wa serikali za mitaa nchini.
Rais alisema: ”Nampongeza Waziri Ghasia kwa kuchukua hatua na mimi
namuunga mkono jambo hilo limetekelezwa kwa baraka zangu, aliniletea
mapendekezo ya uamuzi wake huo na mimi niliandika ‘naunga
mkono,’”alisema Rais Kikwete.
Alisema hivyo ndivyo inatakiwa kwa watumishi wa umma wanaozembea kazi
kuwajibishwa kwa mujibu wa kanuni za maadili ya utumishi wa umma na
kwamba kwa hatua hizo, ni wazi zitakuwa fundisho kwa wengine na hata
kwenye uchaguzi mkuu ujao.
“Hili ni fundisho na tunataka wajue kwamba wenyewe wapo, na
watawawajibisha na nimeongea na wakuu wa vyombo vya juu vya ulinzi
wawawajibishe na wawatie nguvuni wavunjifu wa amani kwenye uchaguzi
huo,” alisisitiza Rais Kikwete.
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz,
ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali
na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715
221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.
No comments:
Post a Comment