Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue.
SIKU moja baada ya Rais Jakaya Kikwete kutengua uteuzi wa Waziri wa
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, Katibu
Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue naye ametangaza kumsimamisha kazi kwa
muda Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliachim Maswi.
Kwa mujibu wa taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu,
Maswi amesimamishwa ili kupisha uchunguzi wa tuhuma dhidi yake, kama
ilivyoelekezwa na Rais Kikwete juzi wakati anahutubia taifa kupitia
wazee na wakazi wa Dar es Salaam kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee.
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz,
ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali
na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715
221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.
Imeeleza kuwa, Balozi Sefue amemsimamisha kazi Maswi kuanzia jana kwa
kutumia madaraka aliyonayo kama Mamlaka ya Nidhamu kwa Watumishi wa
Umma wanaoteuliwa na Rais, wakiwemo Makatibu Wakuu.
Taarifa hiyo ilisema Balozi Sefue amechukua hatua hiyo; “Kwa mujibu
wa Kifungu 4(3) (d) cha Sheria ya Utumishi wa Umma, Na. 8 ya mwaka 2002
(kama ilivyorekebishwa)” ambapo “Katibu Mkuu Kiongozi ndiye Mamlaka ya
Nidhamu kwa Watumishi wa Umma wanaoteuliwa na Rais, wakiwemo Makatibu
Wakuu.”
Badala yake, Balozi Sefue amesema kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya
Nishati na Madini, Ngosi Mwihava atakaimu nafasi ya Katibu Mkuu, Wizara
ya Nishati na Madini hadi uchunguzi dhidi ya Maswi utakapokamilika.
Taarifa hiyo ya Balozi Sefue pia imekariri kauli ya Rais Kikwete
katika hotuba yake kwa Taifa juzi, ambapo Rais alisema: “Kuhusu Katibu
Mkuu wa Wizara ya Nishatina Madini, kwa vile ni Mtumishi wa Umma,
anatawaliwa na Sheria na Kanuni za Utumishi wa Umma, hivyo
nimeshaelekeza Mamlaka kuchunguza tuhuma zake na hatimaye ikibainika ana
makosa hatua za kinidhamu zitachukuliwa.”
Maswi, aliyekuwa Mwanasheria Mkuu Frederick Werema na Mawaziri
wawili, Profesa Tibaijuka na Profesa Sospeter Muhongo wa Wizara ya
Nishati na Madini, walituhumiwa wakati wa Kikao cha Bunge kilichopita
kuhusu Akaunti ya Tegeta Escrow.
Wakati Werema alijiuzulu kutokana na sakata la Escrow kwa kile
alichoeleza kuwa ushauri wake haukuelewa, Tibaijuka ameng’olewa huku
Muhongo akiwekwa kiporo na Rais ili kupisha uchunguzi dhidi yake. Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz,
ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali
na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715
221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.
Akizungumza juzi baada ya kutangaza kumweka pembeni Tibaijuka, Rais
Kikwete alisema; “Kuhusu Muhongo tumemuweka kiporo, kuna uchunguzi
nimeagiza ufanywe na matokeo yake yanaweza kuja baada ya siku mbili na
nitafanya uamuzi wa haki”.
Maswi na Muhongo walikuwepo ukumbini wakati Rais anahutubia, ilhali
Profesa Tibaijuka hakuwepo. Wakati huo huo, Rais Kikwete ameelekeza kuwa
pamoja na hatua nyingine zinazochukuliwa, Shirika la Umeme (TANESCO)
waendelee na majadiliano na IPTL kuhusu uwezekano wa kushusha tozo la
uwekezaji (capacity charge) zaidi ya punguzo la awali, lililopatikana
kupitia Kituo cha Kimataifa cha Kusuluhisha Migogoro ya Kimataifa
(ICSID).
Hatua zinazochukuliwa na Serikali ni ahadi ya Rasia Kikwete wa
kuyafanyia kazi maazimio ya Bunge wakati wa Mkutano wa 16 na 17 wa Bunge
uliomalizika Novemba 28 mjini Dodoma baada ya kutawaliwa na mjadala
mzito wa sakata la Akaunti ya Escrow, ikielezwa baadhi ya ‘wazito’
walichota fedha za umma, jambo ambalo juzi Rais Kikwete aliliweka wazi
hazikuibwa, bali ni mali ya kampuni ya Kampuni ya Kufua Umeme ya
Independent Power Tanzania Limited (IPTL) iliyokuwa katika mzozo wa
kibiashara na Shirika la Umeme Nchini (Tanesco).
Alifafanua kwa kusema: ”Baada ya kuwa na mzozo baina ya Tanesco na
IPTL, waliamua kufungua akaunti ambayo fedha zitakuwa zinahifadhiwa huko
wakati mzozo wao wakiendelea kuutafutia suluhu na akaunti hiyo
waliifungua Julai 5, mwaka 2006”.
Kwamba fedha zilizokuwa zikiwekwa humo ni za madai ya tozo la
uwekezaji, ambalo IPTL iliidai Tanesco hivyo, fedha hizo ni za IPTL na
sio za Umma na kwamba Mamlaka ya Mapato nchini (TRA), ilishapeleka madai
ya kodi ya serikali ya ongezeko la thamani kwa IPTL na wamekubali
kulilipa.
“Kwa mantiki hiyo fedha sio za umma ni za IPTL ambaye ndiye mlipwaji
madai yake kutoka Tanesco,” alisema Rais Kikwete na kuongeza tangu
akaunti hiyo tangu ifunguliwe miaka saba sasa, kwa bahati mbaya Tanesco
haikufanikiwa kufikia suluhu na IPTL hadi kampuni hiyo ikapewa malipo
yake.
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz,
ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali
na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715
221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.
Na Habari Leo
No comments:
Post a Comment