Mahakama
ya kijeshi Mashariki mwa Jamuhuri ya Demokrasi ya Congo imemhukumu kifo
Kanali Birocho Nzanzu baada ya kubainika na makosa ya kutaka kumuua
afisa wa jeshi la nchi hiyo aliyekuwa mstari wa mbele kutokomeza
wapiganaji wa M23.
Afisa anayedaiwa kupangiwa
njama za kuuawa ni Mamadou Ndala mabaye kwa kiasi kikubwa aliamini
katika vita dhidi ya kundi hilo la wapiganaji na ambaye aliuawa mwezi
januari mwaka huu. Hata hivyo hukumu hiyo imetolewa kwa watuhumiwa nane
ambapo kati ya hao mmoja ndiye Kanali Ndala aliyehukumiwa kifo. Mahakama
imebainisha kuwa Kanali Nzanzu amekuwa akitumiwa na waasi wa ADF kutoka
Uganda kuandaa maujaji. Asante
kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza
kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya
neno Jambo TzTuesday, November 18, 2014
GAVANA ATANGAZA HALI YA HATARI, MISSOURI
Gavana
wa jimbo la Missouri nchini Marekani ametangaza hali ya hatari kabla ya
kutolewa uamuzi muhimu kuhusu kumfungulia mashitaka ya jinai au la
dhidi ya afisa wa polisi mzungu, ambaye alimuua kwa kumpiga risasi
kijana wa Kiafrika ambaye hakuwa na silaha.
Mauaji hayo
yaliyotokea katika mji wa Ferguson mwezi Agosti yalisababisha vurugu
katika mitaa kwa siku kadha na kuamsha mjadala kuhusu uhusiano kati ya
polisi na jamii ya watu weusi nchini Marekani.Idara ya polisi ya Kaunti ya St. Louis ndiyo wanaosimamia maandamano yoyote. Meya wa St. Louis, Francis. Slay, amezungumzia kuhusu tahadhari wanayochukua. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Monday, November 17, 2014
MKAPA ATAKA WAZEE NCHINI WASIBEZWE
Rais Mstaafu, Benjamini Mkapa, amewataka
viongozi na Watanzania kutobeza busara na hekima za wazee kwa kuwa bado
wana mchango mkubwa kwa Taifa.
Kadhalika mkuu huyo wa zamani wa nchi, alisema
kuwa, mzee kuota mvi kichwani haina maana ya kupungukiwa na hekima na
maarifa kama wengi wanavyofikiria
Mkapa alitoa kauli hiyo juzi jioni wakati mahafari
ya kwanza ya Shule ya Sekondari ya St Peter Claver iliyoko nje kidogo
ya Mji wa Dodoma.
Alisema anashangazwa kuona maeneo mengi wazee wanapuuzwa na kudharauliwa kama vile hawana mchango wowote kwa maendeleo ya jamii. Asante
kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza
kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya
neno Jambo Tz
PROF. MAGHEMBE ASEMA URAIS SIO MASHINDANO YA UREMBO
Waziri wa Maji, Prof Jumanne Maghembe akizungumza na waandishi wa habari
wa gazeti hili, walipomfanyia mahojiano maalumu ofisini kwake mjini
Dodoma, hivi karibuni.
Waziri wa Maji, Profesa Jumanne Maghembe
ameshangazwa na utitiri wa watu wanaotaka kugombea urais kwenye
Uchaguzi Mkuu 2015, akisema nafasi hiyo ya juu nchini haifanani na
mashindano ya urembo ambayo mtu yeyote anaweza kujaribu.
Mbunge huyo wa Mwanga alisema watu hao
wanaojitokeza kuwania urais hawaelezi wanataka kulifanyia nini Taifa na
akashauri wasioweza kueleza hoja zao wasichaguliwe kushika nafasi hiyo.
“Urais unahitaji kuwa na sifa, dira na ajenda kwa
Taifa,” alisema Profesa Maghembe wakati wa mahojiano maalumu na gazeti
hili mjini hapa.
Kauli ya Profesa Maghembe imekuja wakati Taifa
likijiandaa kwa Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba, 2015, huku chama
chake, CCM kikikabiliwa na kazi ngumu ya kumpata mrithi wa Rais Jakaya
Kikwete ambaye anamaliza muda wake. Asante
kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza
kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya
neno Jambo Tz
SHY-ROSE, SPIKA ZZIWA KIKAANGONI TENA
Bunge la Afrika Mashariki (Eala)
limeitishwa tena, zamu hii jijini Nairobi, Kenya ambako litakutana
kuanzia leo mchana, huku kukiwa na shinikizo kubwa kutoka kwa wabunge 32
linalotaka kung’olewa kwa Spika wa Bunge hilo, Dk Margaret Zziwa na
kuwajibishwa kwa mbunge kutoka Tanzania, Shy-Rose Bhanji.
Bunge hilo linakutana baada ya kuahirishwa kwa
muda usiojulikana kutokana na kukosekana kwa mwafaka baina ya wabunge
kwa upande mmoja na baadhi ya wabunge na Spika Zziwa kwa upande mwingine
lilipokutana Kigali, Rwanda hivi karibuni. Asante
kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza
kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya
neno Jambo Tz
WAZIRI AJIUZULU KUPISHA UCHUNGUZI
Waziri
wa mambo ya ndani wa Ureno amejiuzulu kupisha uchunguzi kuhusu tuhuma
za rushwa inayohusishwa na utoaji vibali vya mgawo wa makazi.
Miguel Macedo amesema hahusiki na kashfa hiyo lakini anajiuzulu kulinda heshima ya taasisi za serikali.Polisi wamewakamata watu 11, akiwemo mkuu wa idara ya uhamiaji nchini humo, siku ya Alhamisi.
Ureno inatoa visa za daraja la kwanza kwa wageni wanaotaka kuwekeza nchini humo.
Mnufaika mkuu wa uharakishaji wa vibali ni raia wa China ambao wamekuwa wakiwekeza kiasi kikubwa nchini Ureno.
Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
MAFUA YA NDEGE YATHIBITISHWA UINGEREZA
Mlipuko
wa mafua ya ndege umethibitishwa katika shamba moja la kuzalishia bata
mashariki mwa Yorkshire, nchini Uingereza, wamesema maafisa.
Wizara
ya Mazingira, Chakula na Masuala ya Vijijini (Defra) imesema hatari kwa
afya ya umma ni ndogo sana. Ndege wasiohitajika wanaondolewa kutoka
eneo hilo na eneo la kuwatenga limeandaliwa.Tatizo hilo bado halijathibitishwa, lakini aina ya kirusi cha H5N1 hakijaweza kubainishwa na maafisa wa Defra.
Kirusi hicho husambaa kati ya ndege na katika matukio ya nadra, kinaweza kuwaathiri binadamu.
Sunday, November 16, 2014
MTOTO ANAYEDAIWA KUGEUKA NYOKA AZUA KIZAA ZAA
Mtoto mchanga mwenye
umri wa miezi minne amezua kizaazaa cha aina yake, baada ya kuwapo
taarifa kwamba mara kadhaa umbo lake limekuwa likigeuka na kuwa nyoka na
mwili wake ukiendelea kudhoofu kutokana na kukataa kunyonya maziwa ya
mama yake.
Mtoto huyo (jina lake tunalihifadhi kwa sasa),
wiki iliyopita alivuta umati wa wakazi wa Kijiji cha Nkome mkoani Geita
ambao walifurika ndani na nje ya Kanisa la AICT Nkome, lililopo kijiji
hapo, kushuhudia maombi ambayo alikuwa akifanyiwa ili kumkomboa katika
kile kilichotafsiriwa kuwa ni mateso dhidi yake.
Ilikuwa saa 4.00 asubuhi Jumamosi, Novemba 8 mwaka
huu wakati mtoto huyo alipofikishwa katika kanisa hilo na kuanza
kufanyiwa maombi na sababu ya hatua hiyo ikielezwa kuwa ni kutokana na
kuwa na umbo la nyoka na kwamba matendo yake yanaashiria kwamba mwenye
asili ya nyoka ndani ya roho yake. Asante
kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza
kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya
neno Jambo Tz
MBOWE AILIPUA SERIKALI KUHUSU BANDARI BUBU NCHINI
Mwenyekiti wa Chacha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe. PICHA|MAKATBA
Mwenyekiti wa Chacha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe amesema kuwa uwepo wa
bandari bubu zinazopitisha bidhaa kwa magendo kutoka nje ni miongoni mwa
sababu zinazoua viwanda vya sukari hapa nchini.
Amesema kuwa viwanda vya miwa vinapokufa,
wanaoumia siyo wenye viwanda bali wakulima wa miwa. Mbowe alisema hayo
juzi alipohutubia mamia ya wafuasi wa chama hicho mjini Turiani , Mkoa
wa Morogoro katika siku ya kwanza ya ziara yake mkoani humo.
Ziara hiyo ni ya Operesheni Delete CCM (ODC) yenye
lengo la kuvihamasisha vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi
(Ukawa), kuiondoa CCM madarakani kuanzia katika Uchaguzi wa Serikali za
Mitaa. Asante
kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza
kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya
neno Jambo Tz
PINDA AHIMIZA KUCHANGIA ELIMU
Waziri Mkuu,
Mizengo Pinda ametoa rai kwa Watanzania kujenga utamaduni wa kuchangia
maendeleo ya sekta ya elimu, badala ya kujikita kuchangia sherehe za
harusi.
Kauli hiyo ilitolewa jana na Naibu Waziri wa Afya
na Ustawi wa Jamii, Dk Stephen Kwebwe aliyezungumza kwa niaba ya Pinda
katika sherehe ya kuchangia ujenzi wa mabweni ya Shule ya Sekondari
Mwenyeheri Anuarite iliyopo Makoka, jijini Dar es Salaam.
“Urithi pekee kwa watoto wetu ni elimu, unaweza
kumwachia mali, lakini itakwisha, ukimwachia elimu hakika huu ndiyo
urithi pekee…: Watanzania wenzangu, tujitoe kuchangia sekta ya elimu
kama ambavyo tunafanya katika sherehe,” alisema Kebwe akiongeza:
“Utamkuta mtu anachangia fedha nyingi katika
harusi na kama tunavyojua harusi moja, ukianza na ‘send off’, ‘kitchen
part’ na harusi yenyewe ni fedha nyingi, lakini mtu huyo huyo ukimwambia
achangie masuala ya elimu, hutamwona.”
Naye Paroko wa Parokia ya Mtakatifu
Gaudence-Makoka wamiliki wa shule hiyo, Padre Evarist Tarimo, alisema
kuwa malengo ya sherehe hiyo ni kuchangisha Sh250 milioni kwa ajili ya
kukamilisha ujenzi wa bweni la wavulana ili kuondoa adha wanayoipata kwa
sasa.
“Hivi sasa vyumba vya madarasa tunavitumia kama
mabweni, hivyo wanasomea humo na kulala humo humo, jambo ambalo
kitaaluma si zuri. Tunatarajia tutakapomaliza ujenzi huo tutawawezesha
wanafunzi wetu kusoma na kulala katika mazingira mazuri na nina hakika
juhudi za wadau zitaweza kukamilisha ujenzi huu,” alisema. Habari
tulizozipata baadaye zilisema jumla ya Sh41.2 milioni zilikusanywa.
Fedha taslimu ni Sh13.3 milioni. Asante
kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza
kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya
neno Jambo Tz
Saturday, November 15, 2014
BUTIKU AMKINGIA KIFUA WARIOBA
Taasisi ya Mwalimu Nyerere
imesema kuwa wanaotaka aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya
Katiba, Jaji Joseph Warioba akae kimya kuhusu Katiba Inayopendekezwa
hawana hoja.
Imesema kuwa wanaosema hivyo hasa wale wa chama
tawala (CCM) wanatakiwa kujiuliza kwa kipindi cha miaka 50 iliyopita
wamefanya nini kuhusu Katiba, ikisisitiza kuwa itaendelea kufanya
midahalo ya kuwaelimisha Watanzania kuhusu mchakato wa Katiba ili
utakapofika wakati wa kura ya maoni waelewe kipi wanatakiwa kukifanya
kwa mustakabali wa taifa.
Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo, Joseph Butiku
alisema hayo jana ofisini kwake jijini Dar es Salaam katika mahojiano
maalumu na gazeti hili kuhusu kazi na majukumu ya Taasisi ya Mwalimu
Nyerere tangu ilipoanzishwa hadi sasa. Asante
kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza
kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya
neno Jambo Tz
G20 YAMUONYA PUTIN AONDOKE UKRAINE
Viongozi wa mataiifa ya magharibi wanaohudhuria mkutano wa mataifa
tajiri, G-20 mjini Brisbane, Australia, wameionya Urusi ifuate
makubaliano ya kusitisha mapigano Ukraine, ama sivyo itakabili vikwazo
zaidi.
Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron, alimwambia Rais
Putin kuwa uhusiano baina ya Ulaya na Urusi utabadilika iwapo wanajeshi
wa Urusi watabaki Ukraine.Rais Obama alisema hatua za Urusi zinachusha.
Urusi inakanusha kuwa ina wanajeshi wake ndani ya Ukraine.
Msemaji wa Bwana Putin alitoa maanani ripoti kuwa kiongozi wa Urusi anapanga kuondoka mapema kwenye mkutano. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
EBOLA YAISHA DRC, YAONGEZEKA S-LEONE
Jamhuri ya Demokrasi ya Congo imejitangaza kuwa haina tena virusi vya
ebola baada ya virusi kuambukiza watu kwa miezi mitatu na kuuwa wagonjwa
karibu 50.
Virusi vya Ebola vilivyoathiri Congo ni tofauti na vile vya Afrika Magharibi.Lakini Waziri wa Afya, Felix Kabange Numbi, amewasihi watu bado kuwa macho - kwamba kumalizika kwa ugonjwa, haimaanishi kuwa nchi haiko kabisa hatarini.
Na Daktari wa Sierra Leone ambaye ameambukizwa Ebola amepelekwa Marekani kwa matibabu.
Martin Salia, ambaye ana kibali cha makaazi Marekani na ambaye ameoa Mmarekani, atatibiwa wakati ametengwa kwenye kitengo maalumu katika jimbo la Nebraska.
Haijulikani iwapo Dr Salia, daktari wa upasuaji, aliuguza wagonjwa wa Ebola Sierra Leone.
Hospitali alikofanya kazi haina kituo cha kuuguza wagonjwa kama hao.
Dakta Salia atakuwa mgonjwa wa 10 wa Ebola kuuguzwa Marekani.
Hadi sasa watu zaidi ya 5,000 wamekufa kutokana na Ebola Afrika Magharibi.
Juma hili iliripotiwa kwamba wakati idadi ya maambukizi ya Ebola yanapungua Liberia na Guinea, bado yanaongezeka nchini Sierra Leone.
Na katika tukio jengine, Ufaransa imewashauri raia wake wasiende katika sehemu fulani za Mali baada ya watu watatu kufariki huko kwa sababu ya Ebola.
Raia wa Ufaransa walioko Mali wameambiwa wafuate ushauri wa serikali ya Mali. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Subscribe to:
Posts (Atom)