Rais Mstaafu, Benjamini Mkapa, amewataka
viongozi na Watanzania kutobeza busara na hekima za wazee kwa kuwa bado
wana mchango mkubwa kwa Taifa.
Kadhalika mkuu huyo wa zamani wa nchi, alisema
kuwa, mzee kuota mvi kichwani haina maana ya kupungukiwa na hekima na
maarifa kama wengi wanavyofikiria
Mkapa alitoa kauli hiyo juzi jioni wakati mahafari
ya kwanza ya Shule ya Sekondari ya St Peter Claver iliyoko nje kidogo
ya Mji wa Dodoma.
Alisema anashangazwa kuona maeneo mengi wazee wanapuuzwa na kudharauliwa kama vile hawana mchango wowote kwa maendeleo ya jamii. Asante
kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza
kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya
neno Jambo Tz
“Wazee wasibezwe wala kupuuzwa, kwani mvi zao kichwani siyo ishara ya kuishiwa busara na hekima,” alisema Mkapa.
Aliwataka wanafunzi na watu wengine kujenga tabia
ya kusoma zaidi na kudadisi mambo ili wawe na uelewa mpana wa kuisaidia
nchi yao katika mambo mbalimbali ya maendeleo.
“Tumekosa utamaduni wa kupenda kujisomea, watu ni
wavivu, hawataka kusoma. Naomba tupende kusoma kwa faida yetu binafsi na
hata Taifa,” alisema.
Alisema kuwa elimu ya kidato cha nne siyo mwisho
wa kupata mafanikio, bali ni mwanzo wa kufikiria na kuona mbali zaidi
ili kufikia malengo ya kuelemika.
Hata hivyo, kiongozi huyo alisisitiza zaidi vijana kupenda kusoma masomo ya sayansi.
“Kuna shida ya wanafunzi wa masomo ya sayansi, hii
inakwanza maendeleo ya Taifa. Jitokezeni msome masomo haya ili
muikomboe Tanzania,” alisema.
Katika mahafali hayo, Mkapa alichanga Sh5 milioni kwa ajili ya kuimaisha maabara ya shule hiyo.
Kwa upande wake, Mkuu wa shule hiyo Padre James
Ayaga, alitaja moja ya changamoto wanazokabiliana Aliwaomba wazazi kuendelea kuchangia na kuisaidia shule hiyo ili iweze
kufikia ndoto zake kwa kutoa wanafunzi wengi wa masomo ya sayansi.nazo kuwa ni pamoja na
ukosefu wa vifaa vya kutosha vya maabara. Asante
kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza
kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya
neno Jambo Tz
No comments:
Post a Comment