Bunge la Afrika Mashariki (Eala)
limeitishwa tena, zamu hii jijini Nairobi, Kenya ambako litakutana
kuanzia leo mchana, huku kukiwa na shinikizo kubwa kutoka kwa wabunge 32
linalotaka kung’olewa kwa Spika wa Bunge hilo, Dk Margaret Zziwa na
kuwajibishwa kwa mbunge kutoka Tanzania, Shy-Rose Bhanji.
Bunge hilo linakutana baada ya kuahirishwa kwa
muda usiojulikana kutokana na kukosekana kwa mwafaka baina ya wabunge
kwa upande mmoja na baadhi ya wabunge na Spika Zziwa kwa upande mwingine
lilipokutana Kigali, Rwanda hivi karibuni. Asante
kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza
kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya
neno Jambo Tz
Kikao hicho kilichoahirishwa Oktoba 30,
kilishindwa kujadili muswada hata mmoja kama ilivyokusudiwa kutokana na
kuwapo kwa shinikizo la baadhi ya wabunge ambao walitaka Shy-Rose
aadhibiwe kwa kile kinachodaiwa ni utovu wa nidhamu aliouonyesha wakati
wa ziara ya viongozi wa Bunge hilo nchini Ubelgiji.
Hata hivyo, mjadala huo uliotokana na hoja ya
Mbunge wa Uganda, Dorah Byamukama kutofikia hitimisho baada ya baadhi ya
wabunge wa Tanzania kutoka nje na kusababisha akidi kukosekana wakati
wa kufanya uamuzi, hivyo Shy-Rose kuponea tundu la sindano.
Wakati kukiwa na mtanziko huo, taarifa ya Eala
inaonyesha kuwa Bunge hilo sasa litakutana tena kwa wiki mbili kuanzia
leo hadi Alhamisi, Desemba 5, mjini Nairobi na litafunguliwa rasmi kesho
Jumanne na Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta.
Taarifa hiyo inasema miswada miwili wa Vyama vya
Ushirika wa 2014 na ule unaohusu Usimamizi wa Sheria kwenye mipaka pia
wa 2014 inatarajiwa kujadiliwa na kupitishwa sambamba na kuwasilishwa
kwa taarifa za kamati mbalimbali za bunge hilo.
Kadhalika wabunge hao wanatarajiwa kushiriki
katika mkutano wa Novemba 29 na 30, ukiwashirikisha Wakuu wa Nchi za
Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), utakaofanya mapitio na kujadili
mpango wa miundombinu.
Hata hivyo, kuna wasiwasi iwapo kazi hizo
zitafanyika kama inavyokusudiwa kutokana na Kamisheni (Tume) ya uongozi
wa Bunge kutokuwa na uwezo wa kufanya uamuzi wowote wa kisheria ikiwa ni
pamoja na kupanga ratiba, kutokana na makamishna wake watano kujiuzulu
mwishoni mwa mwezi jana. Asante
kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza
kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya
neno Jambo Tz
Kujiuzulu kwa makamishna hao wawili kutoka Rwanda,
wawili wa Burundi na mmoja wa Kenya pamoja na wenyeviti wanne kati ya
sita wa Kamati za Eala, kunatokana na mgogoro uliopo ambao unamhusisha
Spika Zziwa na Shy-Rose.
Ofisa Uhusiano Mwandamizi wa Eala, Bobi Odiko
akizungumza na gazeti hili mwishoni mwa wiki alisema: “Ni kweli kwamba
kamisheni haiwezi kufanya uamuzi wowote kutokana na akidi kutotimia
baada ya wajumbe wengine kujiuzulu, lakini Bunge lenyewe litakapokutana
litaamua jinsi ya kujiendesha.”
Aliongeza: “Kwa jinsi hali ilivyo ni lazima
lifanye kazi ya kuunda upya kamisheni ili iweze kupanga utaratibu wa
uendeshaji wa shughuli zake, maana kwa idadi ya makamishna waliopo
hawawezi kufanya kazi, labda kama watakutana kushauriana mambo madogo
madogo ambayo siyo ya kiuamuzi.”
Kitakachofanyika
Kwa msingi huo, Spika Zziwa atakuwa na mtihani mwingine wa
kuzima jaribio la kumwondoa kwenye kiti chake kwani shughuli za awali za
bunge hilo zitapangwa ndani ya vikao vya wabunge wote badala ya
Kamisheni kama ilivyo ada.
Hiyo itakuwa ni fursa kwa wabunge 32 ambao
wamekuwa kinyume na Spika Zziwa kwa muda mrefu kufufua ajenda tatu;
kwanza ni ile ya kubadili kanuni za uendeshaji wa shughuli za Eala,
pili, kutumia kanuni hizo kuanzisha upya mchakato wa kumwondoa Spika na
tatu, kuhitimisha mchakato wa kutoa adhabu kwa Shy-Rose.
Mambo hayo matatu yamo katika maazimio ya wabunge
32 waliokutana Kigali muda mfupi baada ya kuahirishwa kwa kikao chao cha
Eala, Oktoba 30, 2014 na kutamka bayana kwamba hawana imani na Zziwa
hivyo waliazimia suala la kung’olewa kwake litakuwa ajenda ya dharura.
Katika azimio la pili, wabunge hao wanakusudia
kurejesha hoja ya Aprili Mosi, mwaka huu ya kumwondoa spika huyo katika
nafasi yake na katika azimio lao la tatu wabunge hao walikubaliana
kuendelea na hoja iliyowasilishwa na Byamukama ya kutaka Bhanji
awajibishwe kwa utovu wa nidhamu.
Katika azimio la mwisho, wabunge hao waliunda
kamati ya watu watano na katibu ambayo ilipewa jukumu la kuandaa mpango
wa kurejesha heshima, thamani na sifa nzuri kwa Bunge hilo. Katibu wa
Kamati hiyo ni Mbunge wa Tanzania, Nderakindo Kessy.
Bunge la Afrika Mashariki linaundwa na wabunge 52,
kati ya hao 45 ni wa kuchaguliwa na wengine ni maofisa wa Serikali
wakiwamo mawaziri kutoka nchi wanachama wa EAC pamoja na watumishi wakuu
wa Sekretarieti ya jumuiya hiyo. Asante
kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza
kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya
neno Jambo Tz
No comments:
Post a Comment