Mwenyekiti wa Chacha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe. PICHA|MAKATBA
Mwenyekiti wa Chacha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe amesema kuwa uwepo wa
bandari bubu zinazopitisha bidhaa kwa magendo kutoka nje ni miongoni mwa
sababu zinazoua viwanda vya sukari hapa nchini.
Amesema kuwa viwanda vya miwa vinapokufa,
wanaoumia siyo wenye viwanda bali wakulima wa miwa. Mbowe alisema hayo
juzi alipohutubia mamia ya wafuasi wa chama hicho mjini Turiani , Mkoa
wa Morogoro katika siku ya kwanza ya ziara yake mkoani humo.
Ziara hiyo ni ya Operesheni Delete CCM (ODC) yenye
lengo la kuvihamasisha vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi
(Ukawa), kuiondoa CCM madarakani kuanzia katika Uchaguzi wa Serikali za
Mitaa. Asante
kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza
kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya
neno Jambo Tz
“Katika Ukanda wa Pwani ya Bahari ya Hindi, kuna
bandari bubu katika maeneo mengi. Bidhaa kutoka nje ikiwemo sukari
zinaingizwa kwa magendo na kuuzwa kwa bei ya chee. Je, sukari ya Mtibwa
itapata soko?” alihoji Mbowe.
Alisema kuwa sababu nyingine za kusuasua kwa
viwanda hivyo ni Serikali kutoa vibali vya kuingiza sukari kutoka nje
bila kulipia kodi.
“Viwanda vyetu vya sukari vitashindana vipi kwenye
soko kama kukiwa na sukari inayoingizwa kwa kusamehewa kodi huku
nyingine ikiingizwa kwa magendo? Ni wazi viwanda vitakufa na wakulima
kuendelea kuwa maskini,”alisema Mbowe.
Alisema kwamba Serikali haina sera nzuri za
kulinda viwanda vya wawekezaji wa ndani na kuwa hali hiyo ikiendelea,
maisha ya wakulima yataendelea kuwa magumu.
Mwenyekiti huyo alisema viongozi wa Serikali hata
wakiwa bungeni wakihojiwa kuhusu matatizo yanayowakabili wananchi.
hawasemi ukweli.
“Bungeni mawaziri hawasemi ukweli wanapojibu
maswali kuhusu matatizo ya wananchi. Wengine tunashindwa kuzuia hasira
zetu, ndiyo maana tunaona ni bora kwenda kufanya mikutano kwa wananchi,”
alisema Mbowe.
Naye Mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Morogoro, Suzan
Kiwanga aliwataka wananchi wa wilaya hiyo kuhamasishana ili waweze
kujiandikisha kwa ajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Mbowe azuiwa asimalize mkutano
Katika hali isiyo ya kawaida, wafuasi wa chama
hicho walitaka Mbowe aendelee kuhutubia, baada ya saa 12.30 jioni, licha
ya sheria kukataza.
Baada ya Mbowe kuwaeleza kwamba muda umeisha na anafunga mkutano, walimjibu kwa pamoja wakisema; “ endelea, endelea.”
Mbowe ambaye alikuwa ameongozana na Naibu Katibu
Mkuu wa Chadema Zanzibar, Salum Mwalimu alisema kuwa hawezi kuendelea
kwa sababu atakuwa anavunja sheria za nchi, lakini akawaahidi atakwenda
siku nyingine kwa ajili ya mkutano.
Wafuasi hao walikubali na kuanza kumsindikiza kwa miguu kutoka katika uwanja huo hadi alipofikia. Asante
kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza
kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya
neno Jambo Tz
Na Mwananchi
Na Mwananchi
No comments:
Post a Comment