Mtoto mchanga mwenye
umri wa miezi minne amezua kizaazaa cha aina yake, baada ya kuwapo
taarifa kwamba mara kadhaa umbo lake limekuwa likigeuka na kuwa nyoka na
mwili wake ukiendelea kudhoofu kutokana na kukataa kunyonya maziwa ya
mama yake.
Mtoto huyo (jina lake tunalihifadhi kwa sasa),
wiki iliyopita alivuta umati wa wakazi wa Kijiji cha Nkome mkoani Geita
ambao walifurika ndani na nje ya Kanisa la AICT Nkome, lililopo kijiji
hapo, kushuhudia maombi ambayo alikuwa akifanyiwa ili kumkomboa katika
kile kilichotafsiriwa kuwa ni mateso dhidi yake.
Ilikuwa saa 4.00 asubuhi Jumamosi, Novemba 8 mwaka
huu wakati mtoto huyo alipofikishwa katika kanisa hilo na kuanza
kufanyiwa maombi na sababu ya hatua hiyo ikielezwa kuwa ni kutokana na
kuwa na umbo la nyoka na kwamba matendo yake yanaashiria kwamba mwenye
asili ya nyoka ndani ya roho yake. Asante
kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza
kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya
neno Jambo Tz
Mtoto huyo alifikishwa kanisani hapo na mama yake
mzazi, Sarah Silasi wakitokea Kijiji cha Ichile, Wilaya ya Sengerema
mkoani Mwanza, ambako alikimbia matukio yanayohusishwa na ushirikina.
Mmoja wa wazee wa kanisa hilo la AIC Nkome, Mathew
Misana anasema: “Alikuwa anatoa ulimi mithili ya nyoka, mwendo wake
anapolala alijizungusha kama nyoka na hata alipojikunja mwili wake
ulikuwa kama unavyoona nyoka.”
Misana anasema matukio hayo na mengine kadhaa
yakiwamo ya ngozi ya mtoto huyo kuwa nyeusi kama ya nyoka aina ya chatu,
yaliwalazimisha ndugu na jamaa zake wakiongozwa na mama mzazi kutaka
aombewe.
“Ngozi yake kuonekana kama ya mzee huku macho yake
yakionekana kuwa makubwa na kichwa chake kuwa na umbo la nyoka pamoja
na miguu, baada ya kuona hali hii tukaihusisha na mambo ya kishirikina
na kuamua kuanza maombi,” alisisitiza.
Hata hivyo, muda mfupi baada ya maombi kuanza,
taarifa za kuwapo kwa aina hiyo ya mtoto zilisambaa haraka na
kusababisha umati mkubwa wa watu kujaa ndani ya kanisa hilo ambalo ni
boma kwa maana kwamba ujenzi wake bado unaendelea.
“Watu wengi walijaa na wengine wakawa wanapanda
juu ya miti na juu ya boma wakati mwingine matofali yalianguka. Hewa
ikapungua na usalama ukawa mdogo kwani watu walisukumana wakitaka
kushuhudia,” anasema Misana.
Baada ya watu kuwa wengi, uongozi wa kanisa
uliomba msaada wa Polisi wa Kituo cha Nkome ambao walifika kanisani hapo
na kushauri mtoto huyo aonyeshwe ili watu waweze kuridhika kwamba
hakuwa amegeuka kuwa nyoka.
Uongozi wa kanisa ulifanya hivyo lakini mwonekano
wa mtoto huyo ulisababisha watu kuongezeka badala ya kupungua na hapo
ndipo polisi walipoelekeza mama wa mtoto huyo ambebe na kuondoka naye
hadi kituoni.
Mwinjilisti wa kanisa hilo, Emmanuel Misungwi
anasimulia: “Tumeshudia vitu visivyo vya kawaida wakati tunafanya maombi
na wakati tunaendelea na huduma, mama wa mtoto Sarah alianguka akaanza
kuongea juu ya mtoto kwa nguvu ya mapepo.”
Anasema hali hiyo iliwavuta watu wengi kiasi cha usalama wa
mtoto kuwa mdogo, ndipo walipoamua kuomba msaada wa ulinzi kutoka
polisi.
“Ilibidi polisi waingilie kati, walimchukua mtoto
na kuondoka naye na kuwaridhisha wananchi kwa kumwonyesha hadharani ili
kila mtu aone kama kweli ni nyoka kama uvumi ulivyokuwa umeena au la,”
anasema Misungwi.
Kituo cha polisi
Baada ya mama huyo na mwanaye kufikishwa polisi,
umati wa watu ulihamia katika kituo hicho na kuwafanya askari kufanya
kazi ya ziada kuwaondoa watu waliokuwa wamekusanyika katika eneo hilo.
Licha ya wananchi kufukuzwa waliendelea
kun’gang’ania kukaa katika kituo hicho, hali ambayo ilisababisha polisi
kumwondoa mwanamke huyo kwa kificho na kumpeleka nyumbani kwa mchungaji
wa kanisa hilo, Mchungaji Mkuu wa Kanisa hilo Jonh Marko.
Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Nkome, Charles
Belenge alithibitisha kuwepo kwa tukio hilo na kusema kuwa hali hiyo
imesababisha vurugu wakati wa maombi.
“Nikweli tukio hilo lipo la kudai mtoto
anabadilika kuwa nyoka, kwa kweli limetupa shida kwani hali ya utulivu
katika kijiji ilibadilika kwa muda, lakini tumejitahidi kufanya
udhibiti,” anasema Belenge.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Geita, Joseph Konyo
alithibitisha kuwapo kwa tukio hilo na kwamba walikuwa wakilifanyia
uchunguzi wa kina.
“Haya mambo ndiyo yanasababisha mauaji ya mapanga,
hivyo kama Jeshi la Polisi tutafuatilia kujua kwa kina ili lisije
kusababisha madhara ya mauaji ya kukatana kwa mapanga,” alisema Konyo.
Alihusisha tukio hilo na uelewa mdogo wa wazazi na
wachungaji waliokuwa wakifanya maombi na kwamba mtoto huyo huenda
alikuwa anasumbuliwa na maradhi ya utapiamlo, tofauti na mawazo kwamba
tatizo ni nguvu za giza.
“Kazi tunayoifanya kama Jeshi la Polisi ni kuweka
ulinzi kwa kuzuia wasifanye maombezi eneo la kanisa hilo ambalo kiukweli
liko wazi sana kwani usalama utakuwa mdogo pia tuombe wanaohusika
wampeleke mtoto hospitali,” alisema Konyo.
Mashuhuda wa maombi
Misana anasema wakati wakifanya maombi mtoto huyo alikuwa hatoi
sauti isipokuwa alikuwa anatoa ulimi kama ufanyavyo nyoka na kwamba
ulimi huo ulikuwa mrefu mpaka shingoni pamoja na macho yake kuwa
makubwa.
Mashuhuda wengine walisema kuwa waliona mtoto huyo
akigeuka kimaajabu na kuwa na maumbo mithili ya nyoka na baadaye kurudi
katika umbo la binadamu.
“Mimi nimeona wakati anaombewa alikuwa anatoa
ulimi kama nyoka, alikuwa anasimamisha kichwa na kutoa ulimi hadi
unagusa shingo halafu tumbo, miguu na kiuno vilizunguka,” anasimulia
mkazi wa Nkone, Shaban Masembe.
Naye Neema Masatu anasema: “Niliambiwa Kanisa la
AIC kuna mtoto anabadilika kuwa nyoka anafanyiwa maombi ikabidi nije
nijionee, nimefika hapa nikakuta kweli watu wamejigawa makundi mawili;
wengine wanamuombea mama wa mtoto na wengine mtoto.”
Masatu anafafanua kuwa alichokiona si nyoka
isipokuwa ameona mtoto huyo akiwa anatembea kama nyoka, anajikunja miguu
inagusa shingo kisha kichwa anakisimamisha kama nyoka na kutoa ulimi
mrefu na mdomo na macho yake yalikuwa yanakuwa makubwa.
Naye Pili Nyachimb’huga anasema: “Sijaona, watu
walikuwa wengi nimefika hapa hata sikuweza kumuona ila watu wanasema
alikuwa mtu anayefanana na nyoka, alikuwa anaachama kama nyoka na kwamba
alikuwa anatanuka mwili wake unakuwa mkubwa”.
Ni ipi historia ya mtoto huyu? Usikose toleo
lijalo ambapo mama mzazi atazungumzia kwa undani sababu za mtoto wake
kuwa na matendo yanayofanana na ya nyoka. Asante
kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza
kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya
neno Jambo Tz
No comments:
Post a Comment